Habari za Punde

Shirika la WoteSawa lazindua mradi wa “Paza Sauti ya Mfanyakazi wa Nyumbani” wilayani Ilemela

Shirika la kutetea haki za watoto wafanyakazi wa nyumbani WoteSawa lenye makazi yake Jijini Mwanza, leo limezindua mradi wa kuwajengea uwezo wafanyakazi wa nyumbani katika Manispaa ya Ilemela ili kutetea haki na maslahi yao. Akizungumza kwenye uzinduzi wa mradi huo uitwao “Paza Sauti ya Mfanyakazi wa Nyumbani”, Mkurugenzi wa shirika hilo Angel Benedicto amesema mradi huo pia utawasaidia wafanyakazi wa nyumbani kufichua changamoto zinazowakabiri. Mkurugenzi wa WoteSawa, Angel Benedicto akizungumza kwenye uzinduzi/ utambulisho wa mradi huo uliofanyika Monarch Hotel Mwanza. Wadau walioshiriki uzinduzi huo wakimsikiliza Mkurugenzi wa shirika la WoteSawa, Angel Benedicto Wadau walioshiriki uzinduzi huo wakimsikiliza Mkurugenzi wa shirika la WoteSawa, Angel Benedicto Diwani wa Kata ya Kitangiri Manispaa ya Ilemela, Elizabert Wangaluka akizungumza wakati wa utambulisho wa mradi huo. Rehema Mkinza ambaye ni Afisa Ustawi wa Jamii Manispaa ya Ilemela akieleza namna serikali inavyoshiriki ipasavyo katika kupambana na utumikishwaji wa mtoto Washiriki wakifuatilia mada kwenye uzinduzi huo. Mratibu wa Shirika la Kutetea Haki za Wafanyakazi wa Nyumbani (Wotesawa) Elisha David akitambulisha mradi huo.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.