Habari za Punde

“TAHLISO YAIOMBA HESLB KUHARAKISHA FEDHA ZA WANAFUNZI VYUONI”

JUMUIYA wa Wanafunzi wa Elimu ya Juu Tanzania (Tahliso) wameiangukia bodi ya mikopo ya wanafunzi wa elimu ya Juu (HESLB) kuharakisha fedha za wanafunzi waliofeli baadhi ya masomo kwa kupata alama D waliopo vyuoni(supplementary).

Hayo yalisemwa na Mwenyekiti wa Jumuiya hiyo,Stanslaus Kadugalize wakati akizungumza na mtandao huu ambapo alisema idadi ya wanafunzi waliofeli baadhi ya masomo vyuoni ni kubwa na mpaka sasa hawajapata fedha za kujikimu .

Alisema fedha hizo ni kama kauli ya Naibu Waziri wa Elimu alivyosema kuwa ifikapo ijumaa wiki iliyopitia fedha ziwe zimefika vyuoni lakini mpaka sasa fedha hizo hazijafika jambo ambalo linawapa wakati mgumu wanafunzi hao.

Mwenyekiti huyo alivitaka vyuo visiweke sababu zisizo za msingi juu ya kuwapa wanafunzi fedha zao za kujikimu kwa wale ambao tayari fedha zimekwisha fikishwa vyuoni kwa kigezo cha kujisajili.

“Tunatambua umuhimu wa kujisajili ila vyuo vitambue pia kwamba wapo wanafunzi wengi wanategemea fedha hizo hizo za bodi ya mikopo (HESLB) ili kulipia gharama za kujisajili kuweza kukamilisha zoezi la kujisajili hivyo vyuo viache kuweka sababu zinazopelekea usumbufu kwa wanafunzi “Alisema.

Kuhusu zoezi la utoaji wa mikopo kwa wanafunzi wa mwaka wa kwanza alisema sasa bodi ya hiyo imekwisha kutoa kwa wanafunzi 29,000 kwa wale wote ambao wanasifa na hawajapata katika upangaji wa awali aliwashauri kutumia dirisha la rufani linalofunguliwa Novemba 13 mwaka huu ambapo rufaa hizo itakuwa ni bure.

Hata hivyo Mwenyekiti huyo hakisita kuzungumzia kuhusu zoezi la udahili ambapo ambapo aliitaka TCU kuingilia kati kwani bado kuna usumbufu mkubwa wa wanafunzi wanaoupata na una hatarisha baadhi yao kukosa nafasi ya kusoma.

Alisema vipo vyuo vimefahili wanafunzi zaidi ya idadi wanayotakiwa mfano chuo cha Mwenge na vyenginevyo jambo la ajabu wanapokwenda kuripoti vyuoni wanaambiwa wamekwisha kamilisha idadi walizopangiwa.

“Sasa tunajiuliza kwanini walikubali idadi kubwa ya wanafunzi
wathibitishe kwenye vyuo vyao? kwanini wasiweke ukomo wa idadi kulingana na wanayotakiwa  lakini pia mpaka sasa wapo wanasumbuliwa vyuoni hawajapokelewa na wametoka makwao “Alisema.

“Mfano yupo mwanafunzi ametoka kwao Arusha amekwenda Mwanza kuripoti chuo kalipa na ada kabisa ya chuo sikitaji  na alithibitisha kusoma hapo ajabu amekwenda kuripoti wana mwambia wameshajaza idadi hivyo subiri maamuzi ya TCU kama wataruhusu kuwapokea “Alisema.

Aliongeza kuwa vyuo visipelekee vurugu zisizo na maana yoyote ile endapo wanafunzi hao watakosa nafasi za masomo kwa mwaka huu kwa uzembe wa vyuo kudahili zaidi ya idadi yao kwa hofu ya kukosa wanafunzi .

“Lakini niwaambie sisi kama Tahliso hatutasita kuvichukulia hatua vyuo hivyo kwa kuwalipa fidia ya usumbufu wanafunzi  ambao wamekumbana naowakati wa kufuatilia michakato hiyo “Alisema.
Habari kwa Hisani ya Blog ya Kijamii ya Tanga Raha

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.