Habari za Punde

Zanzibar Heroes kuagwa kesho

 Abubakar Khatib Kisandu, Zanzibar.

Timu ya Taifa ya Zanzibar (Zanzibar Heroes), inatarajia kuagwa kesho kwa ajili ya safari yao ya kwenda mjini Kenya, kwenye Mashindano ya CECAFA Chalenj CUP yanayotarajiwa kuanza Disemba 3-17, 2017.
Heroes itaagwa saa 9:00 alaasiri na Waziri wa Habari Utalii Utamaduni na michezo Rashid Ali Juma katika ukumbi wa V.I.P Uwanja wa Amaan.
Katika Mashindano hayo Heroes imepangwa Kundi  A ambalo lina timu za Tanzania Bara, Libya, Rwanda na wenyeji Kenya.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.