Habari za Punde

Askari JWTZ walionusurika shambulio la DRC wanaendelea vizuri

Baadhi ya Wanajeshi wa JWTZ waliojeruhiwa kwenye shambulio nchini DR Congo wakiwa kwenye hospitali ya Goma ambapo wanaendelea kupatiwa matibabu.

KUFUATIA wanajeshi 14 wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi Tanzania (JWTZ), waliouawa katika nchi ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), wakati wakilinda amani kushambuliwa na waasi kuuawa huku wengine 44 wakijeruhiwa na mmoja wao kutojulikana alipo, picha za majeruhi wa tukio hilo zinaoshesha wanaendelea vizuri.


Kiongozi wa Mkuu wa Walinzi wa Amani wa Umoja wa Mataifa Duniani, Jean-Pierre Lacroix amewatembelea ma kuwasalimia Askari Majeruhi wa JWTZ wanaopatiwa matibabu nchini Congo na Uganda baada ya shambulio hilo.
Miili ya wanajeshi waliouawa kwenye shambulio hilo iliagwa juzi Desemba, 14 mwaka huu katika Viwanja vya ulinzi vilivyopo makao ya jeshi yaliyopo Upanga jijini Dar es Salaam.



Mkuu wa operesheni za ulinzi za Umoja wa Mataifa Jean-Pierre Lacroix amewajulia hali walinda amani wawili wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) waliolazwa katika hospital ya Mulago mjini Kampala nchini Uganda.
Wanajeshi waliouawa ni  Hamad Haji Bakari, Chazil Khatibu Nandonde, Idd Abdallah Ally, Juma Mossi Ally,  Ally  Haji Ussi, Pascal Singo, Samwel Chenga, Deogratius Kamili, Mwichumu Vuai Mohamed, Hassan Makame, Issa Mussa Juma, Hamad Mzee Kamna, Salehe Mahembano na Nasoro Haji Bakari.



Mkuu wa operesheni za ulinzi za Umoja wa Mataifa Jean-Pierre Lacroix amewajulia hali walinda amani wawili wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) waliolazwa katika hospital ya Mulago mjini Kampala nchini Uganda.

Askari hao 14 walifariki dunia katika mapigano na waasi wa kikundi cha ADF nchini DRC, huku 44 wakijeruhiwa na mmoja akipotea baada ya kambi yao kuvamiwa eneo la Mashariki mwa nchi Desemba 7 wakati wakitekeleza majukumu ya ulinzi wa amani.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.