Habari za Punde

Hafla ya Upokeaji wa Msaada wa Madawa kutoka Serikali ya Oman

 Waziri wa Afya Mhe,Mahmoud Thabit Kombo kulia akizungumza na Viongozi pamoja na Waandishi wa Vyombo mbali mbali vya Habari katika hafla ya Upokeaji wa Msaada wa Madawa kutoka Serikali ya Oman hafla iliofanyika katika Ukumbi wa Wizara ya Afya Mnazi Mmoja Zanzibar.
 Mwandishi wa Habari wa ITV Farouk Kariym akiuliza maswali kwa Waziri wa Afya Mahmoud Thabit Kombo hayupo pichani baada ya kupokea Msaada wa Madawa kutoka Serikali ya Oman hafla iliofanyika katika Ukumbi wa Wizara ya Afya Mnazi Mmoja Zanzibar.

Waziri wa Afya Mhe,Mahmoud Thabit Kombo katikati akipokea msaada wa madawa aina mbalimbali kutoka Serikali ya Oman uliokabidhiwa na Balozi wa Oman anaefanyia kazi zake Zanzibar Dk,Ahmed Hamood Al-Habsi (kulia yake) hafla iliyofanyika katika Ukumbi wa Wizara ya Afya  Mnazi Mmoja Zanzibar kushoto yake ni Naibu Balozi wa Oman Ahmed Mohammed Al-Muzaini mwengine ni Mfamasia Mkuu wa Wizara ya Afya Habib Ali Sharif na kulia ni Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Afya Halima Maulid Salum.

PICHA NA YUSSUF SIMAI/MAELEZO ZANIZBAR.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.