Habari za Punde

Sherehe za kuwapongeza wachezaji wa Timu ya Zanzibar Heroes uwanja wa michezo Gombani

 VIONGOZI mbali mbali wa Serikali wakiongozwa na Waziri wa Habari Utalii Utamaduni na Michezo Pemba, Mhe:Rashid Ali Juma katikaati, kushoto ni Mshauri wa Rais mambo ya Utalii, utamaduni na Michezo Zanzibar Chimbeni Kheri na kulia ni Kocha mkuu wa Timu ya Taifa ya Zanzibar (Zanzibar Heroes) Hemed Suleiman Moroko, wakiangalia kikundi cha Taifa cha Tarab wakati wa haflan ya kuwapongeza wachezaji wa Zanzibar Heroes iliyofanyika uwanja wa Gombani.(PICHA NA ABDI SULEIMAN, PEMBA)
 VIONGOZI mbali mbali wa Serikali Kisiwani Pemba, wakiongozwa na Afisa Mdhamini wa Habari Utalii Utamaduni na Michezo Pemba, Khatib Juma Mjaja, wakifuatilia kwa makini tarab kutoka kikundi chan Taifa, wakati wa sherehe ya timu ya Zanzibar Heroes katika uwanja wa Gombani.(PICHA NA ABDI SULEIMAN, PEMBA)
 VIONGOZI mbali mbali wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, Wakiongozwa na Waziri wa Wizara ya Habari Utalii, Utamaduni na Michezo Zanzibar, Mhe:Rashid Ali Juma, wakifuatilia kwa makini Tarab ya kikundi cha Taifa Zanzibar. .(PICHA NA ABDI SULEIMAN, PEMBA).
 WAPIGAJI wa magitaa katika kikundi cha Taifa cha Taraba Zanzibar, wakiwajibika katika kazi ili kupata mziki mzuri wa tarab, wakati wa sherehe ya kuwapongeza wachezaji wa Timu ya Taifa ya Zanzibar Heroes tarab iliyofanyika katika uwanja wa michezo Gombani.(PICHA NA ABDI SULEIMAN, PEMBA)
 VIONGOZI wa Serikali wakiongozwa na Naibu Waziri wa Wizara ya habari, Utalii, Utamaduni na Michezo Pemba Mhe:Chumu Kombo Khamis (Katikati), kulia ni kushoto ni Mkuu wa Wilaya ya Micheweni Salama Mbarouk Khatib na kushoto ni Katibu tawala Wilaya ya Mkoani Miza Hassan Faki, wakifuatilia kwa makini kikundi cha Tarab ya Taifa katika uwanja wa Gombani.(PICHA NA ABDI SULEIMAN, PEMBA)
 AFISA Mdhamini Wizara ya habari Utalii, Utamaduni na Michezo Pemba, Khatib Juma Mjaja akitoa maelezo machache juu uwepo wa timu ya Taifa ya Zanzibar (Zanzibar Heroes) Kisiwani Pemba.(PICHA NA ABDI SULEIMAN, PEMBA)
 KOCHA Mkuu wa Timu ya Taifa ya Zanzibar (Zanzibar Heroes) Hemed Suleiman Moroko, akiwatambulisha wachezaji wake katika shehere maalumu ya Tarab ya kuwapongeza wachezaji wa timu hiyo, iliyofanyika katika uwanja wa Michezo Gombani.(PICHA NA ABDI SULEIMAN, PEMBA)
 KOCHA Mkuu wa Timu ya Taifa ya Zanzibar (Zanzibar Heroes) Hemed Suleiman Maroko, akimtunza mmoja wa waimbaji wa kikundi cha Tarab cha Taifa Zanzibar, wakati wakiimba wimbo wa kuipongeza timu ya Zanzibar Heroes katika taarab maalumu iliyofanyika uwanja wa Gombani.(PICHA NA ABDI SULEIMAN, PEMBA)
 WAZIRI wa Habari Utalii, Utamaduni na Michezo Zanzibar, Mhe:Rashid Ali Juma akitoa salamu za Mhe:Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa baraza la Mapinduzi Dk Ali Mohamed Shein, wakati wa sherehe za kuwapongeza wachezaji wa Timu ya Zanzibar Heroes katika uwanja wa michezo Gombani.(PICHA NA ABDI SULEIMAN, PEMBA
MKUU wa Wilaya ya Wete Mhe:Abeid Juma Ali akimtunza mmoja wa waimbaji wa nyimbo ya Taraba, inayojulikana kwa jina la Baba shein Uko sawa ya kuwapongeza wachezaji wa Zanzibar heroes.(PICHA NA ABDI SULEIMAN, PEMBA)

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.