Waziri wa Fedha na
Mipango Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb) (kushoto) akizungumza na waandishi
wa habari kuhusu Hali ya uchumi na
utekelezaji wa Bajeti ya Serikali kwa mwaka 2017/18 ambapo alitoa agizo kwa
vyombo vya ulinzi kuwakamata wanaowalazimisha watanzania kufanya malipo kwa
Dola badala ya Shilingi, mkutano ulifanyika katika ukumbi wa Wizara ya Fedha na
Mipango Jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Fedha na
Mipango Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb) (mbele) akiwa katika Mkutano na
waandishi wa habari kuhusu hali ya uchumi na utekelezaji wa Bajeti ya Serikali
kwa mwaka 2017/18 katika ukumbi wa Wizara ya Fedha na Mipango Jijini Dar es
Salaam.
Naibu Katibu Mkuu
wa Wizara ya Fedha na Mipango Bi. Susana Mkapa na Afisa Mwandamizi wa Wizara
hiyo Bw. John Sausi wakizungumza jambo wakati wa Mkutano kati ya Waziri wa
Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb) (hayupo pichani) na
Waandishi wa Habari kuhusu Hali ya uchumi na utekelezaji wa Bajeti ya Serikali
kwa mwaka 2017/18 katika ukumbi wa Wizara ya Fedha na Mipango Jijini Dar es
Salaam.
Maafisa Waandamizi
kutoka Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) wakifurahia jambo wakati Waziri wa Fedha
na Mipango Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb) (hayupo pichani) alipokuwa
akizungumza na waandishi wa habari ambapo aliangazia suala la hali ya Uchumi na
kubainisha kuwa ni imara ukilinganisha na nchi nyingine za Afrika Mashariki,
katika ukumbi wa Wizara ya Fedha na Mipango Jijini Dar es Salaam.
No comments:
Post a Comment