MELI ya Mv Mapinduzi II ikiwasili katika bandari ya
Mkoani, ikiwa imebeba wachezaji wa Timu ya Taifa ya Zanzibar Heroes na Kikundi
cha Tarab cha Taifa.(PICHA NA ABDI
SULEIMAN, PEMBA.)
VIONGOZI mbali mbali wa Serikali ya Mapinduzi ya
Zanzibar wakiongozwa na Naibu Waziri wa Harabi Utalii,Utamaduni na Michezo
Zanzibar Mhe:Chumu Kombo Khamis, wakuu wa wilaya, Maafisa wadhamini na wananchi
mbali mbali wa Pemba, wakiwasubiri kuwapokea wachezaji wa timu ya Zanzibar
Heroes.(PICHA NA ABDI SULEIMAN, PEMBA.)
MSHAURI wa Rais mambo ya Utamaduni Zanzibar Chimbeni
Kheir, akiteremka katika meli ya Mv Mapinduzi II, iliyowasili katika bandari ya
mkoani na mashujaa wa timu ya Zanzibar Heroes.(PICHA NA ABDI SULEIMAN, PEMBA.)
NAIBU waziri wa Habari, Utalii, Utamaduni na Michezo
Zanzibar, Mhe:Chumu Kombo Khamis, akisalimiana na Mshauri wa Rais mambo ya
Utamaduni Zanzibar Chimbeni Kheir, mara baada ya kuwasili na msafara wa
wachezaji wa timu ya Zanzibar Heroes Katika bandari ya Mkoani.(PICHA NA ABDI SULEIMAN, PEMBA.)
WACHEZAJI wa Timu ya Zanzibar Heroes wakiongozwa na
Kocha makuu wa timu hiyo, Hemed Morocco wakiteremka katika maeli ya Mv Mapinduzi
II katika bandari ya Mkoani, kwa lengo la kucheza mchezo wa kirafiki na Timu ya
Pemba Kombaini.(PICHA NA ABDI SULEIMAN,
PEMBA.)
WACHEZAJI wa Timu ya Taifa ya Zanzibar (Zanzibar
Heroes) wakisalimiana na viongozi mbali mbali wa Serikali ya Mapinduzi ya
Zanzibar, baada ya kuwasili katika bandari ya mkoani kwa ajili ya mchezo wa
kirafiki dhidi ya Pemba Kombaini.(PICHA
NA ABDI SULEIMAN, PEMBA.)
WADAU na Mashabiki mbali mbali wa soka wakiwapokea
na kuwashangiria mashujaa wa Timu ya Taifa ya Zanzibar (Zanzibar Heroes) baada
ya kuwasili katika bandari ya Mkoani.(PICHA
NA ABDI SULEIMAN, PEMBA.)
BRASSBAND ya vijana chipukizi Kisiwani Pemba,
wakiongoza maandamano ya wachezaji na Viongozi wa Timu ya Taifa ya Zanzibar
(Zanzibar Heroes) walipowasili katika bandari ya Mkoani Kisiwani Pemba.(PICHA NA ABDI SULEIMAN, PEMBA.)
No comments:
Post a Comment