Habari za Punde

ZANZIBAR HEROES YAWASILI SALAMA MACHAKOSI KENYA, TAYARI KUCHEZA CHALENJ CUP

Na Abubakar Khatib Kisandu.Machakos Kenya.
Timu ya Taifa ya Zanzibar (Zanzibar Heroes) imefika salama katika Jiji la Machakos nchini Kenya tayari kuanza Mashindano ya CECAFA Chalenj Cup ambayo yanatarajiwa kuanza kesho kutwa Jumapili Disemba 3, 2017.
Jumla ya msafara wa watu 41 wakiwemo wachezaji 24 umewasili jioni ya leo na wamefikia katika Hoteli ya Garnen Hotel iliyopo Machakosi.
Mkuu wa Msafara huo Khamis Ali Mzee amesema wamepokelewa vizuri na uongozi wa CECAFA hivyo imezidi kuwapa ari ya kufanya vizuri katika Mashindano hayo.
“Tunashukuru tumefika salama hapa Kenya, safari ilikuwa ngumu kiasi lakini tunashukuru uongozi wa CECAFA kuja kutupokea, tunaimani vijana watafanya vyema katika Mashindano”. Alisema Mzee.
Heroes wataanza kucheza mchezo wao wa awali Jumanne saa 8:00 za mchana dhidi ya Rwanda.
Benchi la ufundi la Hereos linaongozwa na Hemed Suleiman “Morocco” (Kocha Mkuu), Hafidh Muhidin (Msaidizi), Ali Suleiman “Mtuli” (Msaidizi), Abdulwahab Dau (Meneja), Saleh Ahmed “Machupa” (Kocha wa Makipa)na Abrahmani Ali (Mtunza vifaa).
Wachezaji 24 waliochaguliwa kuwakilisha kikosi hicho ni :-
WALINDA MLANGO
Ahmed Ali "Salula" (Taifa ya Jang'ombe), Nassor Mrisho (Okapi) na Mohammed Abdulrahman "Wawesha" (JKU).
WALINZI
Abdallah Haji "Ninja" (Yanga), Mohd Othman Mmanga (Polisi), Ibrahimm Mohammed "Sangula" (Jang'ombe Boys), Adeyum Saleh "Machupa" (Kagera Sugar), Haji Mwinyi Ngwali (Yanga), Issa Haidar "Mwalala" (JKU), Abdulla Kheir "Sebo" (Azam) na Ibrahim Abdallah (Taifa ya Jang'ombe).
VIUNGO
Abdul-swamad Kassim (Miembeni City), Abdul Aziz Makame (Taifa ya Jang'ombe),Mudathir Yahya (Singida United), Mohd Issa "Banka" (Mtibwa Sugar), Amour Suleiman "Pwina" (JKU) na Hamad Mshamata (Chuoni).
WASHAMBULIAJI
Suleiman Kassim "Seleembe" (Majimaji), Kassim Suleiman (Prisons),  Feisal Salum (JKU),  Khamis Mussa "Rais" (Jang'ombe boys), Mwalimu Mohd (Jamhuri), Seif Abdallah “Karihe” (Lipuli) na Ibrahim Hamad Hilika (Zimamoto).

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.