Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein, akipata maelezo ya uhifadhi wa samaki kwa ajili ya kusafirisha Nje ya Nchi wakati alipotembelea kiwanda hicho akiwa katika ziara yake katika Nchi za Umoja wa Nchi za Kiarabu UAE.
Katika ziara yake mjini
Sharja Dk. Shein alipata fursa ya kutembelea eneo la shughuli za uvuvi la ‘East
Fishing Processing LLC”, lililoko Al Jurf
katika eneo la Ajman na kupata
maelezo juu ya namna ya eneo hilo lenye kiwanda kikubwa cha kisasa cha samaki jinsi
kinavyosarifu na kuhifadhi samaki pamoja
na kuwaweka katika mfumo maalum wa kwa ajili ya kuuzwa.
Kwa mujibu wa Mkurugenzi
Mkuu wa Kampuni hiyo inayolishirikisha kundi la Kampuni ya THOMSUN, K.V. Thomas
alimueleza Rais Dk. Shein namna na kiwanda hicho kinavyosarifu samaki wa aina
mbali mnali wakiwemo kamba kutoka nchi mbali mbali ikiwemo Tanzania.
Dk. Shein kwa upande
wake alipendezewa na namna kiwandaa hicho kinavyofanya kazi na kutokana na
juhudi zinazoendelea kuchukuliwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar katika
sekta ya uvuvi na viwanda vya samaki pamoja na azma ya kuanzisha Kampuni ya
Uvuvi, Rais Dk. Shein alisisitiza haja ya kuwepo kwa mashirikiano ya pamoja ili
Zanzibar ipate kupanua wigo katika sekta hiyo.
Kutokana na kiwanda
hicho kutumia teknolojia ya kisasa katika kusarifu samaki wa aina mbali mbali
pia, soko la ajira limeonekana kuchukua fursa yake kutokana na kuajiri vijana
wengine hatua ambayo Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar imo katika kupambana na
changamoto iliyopo katika suala zima la ajira.
No comments:
Post a Comment