Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein, akizungumza na Gavana wa Banki Kuu ya Tanzania anayemaliza muda wake Profesa Benno Ndulu, alipofika Ikulu Zanzibar leo kumuaga baada ya kumaliza muda wake wa Kazi akiwa na Ujumbe wake.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein, akiwa katika picha ya pamoja na Gavana wa Banki Kuu ya Tanzania anayemaliza muda wake Profesa Benno Ndulu na Maofisa wa BOT, baada ya hafla na ais wa Zanzibar Ikulu Zanzibar.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein, akizungumza na Gavana wa Banki Kuu ya Tanzania anayemaliza muda wake Profesa Benno Ndulu, alipofika Ikulu Zanzibar kwa mazungumzo na kumuaga baada ya kumaliza Muda wake wa Kazi na kustaafu nafasi hiyo.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein, akizungumza jambo baada ya mazungumzo yake na Gavana wa Banki Kuu ya Tanzania anayemaliza muda wake Profesa Benno Ndulu, wakitika ukumbi wa mkutano kwa ajili ya kupiga picha ya kumbukumbu.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein, akiwa katika picha ya pamoja na Gavana wa Banki Kuu ya Tanzania anayemaliza muda wake Profesa Benno Ndulu na Maofisa wa BOT, baada ya hafla na ais wa Zanzibar Ikulu Zanzibar.
RAIS wa
Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein ameagana na
Gavana wa Benki ya Tanzania (BOT) anayemaliza muda wake Profesa Benno Ndulu
ambaye ameeleza furaha yake ya kuuona uchumi wa Zanzibar ukiwa umeimarika kwa
kiasi kikubwa chini ya uongozi wa Dk. Shein.
Katika mazungumzo hayo ya kuagana yaliyofanyika
Ikulu mjini Zanzibar, Profesa Ndulu alimueleza Dk. Shein kuwa kazi ya
kuimarisha uchumi iliyofanywa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar chini ya
uongozi wa Dk. Shein ni kubwa sana na kuna haja ya kupongezwa.
Profesa Ndulu alieleza kuwa uchumi wa Zanzibar ni
mkubwa sana hatua ambayo inatokana na kasi kubwa ya kuimarisha uchumi huo
ilivyofanywa huku akisisitiza kuwa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar iko vizuri
kifedha.
Alieleza kuwa sekta ya utalii nayo kwa upande wake
imeweza kuchangia kwa kiasi kikubwa kuimarisha uchumi wa Zanzibar sekta ambayo
imeweza kusaidia kukuza uchumi huo badala ya kutegemea zao moja la karafuu peke
yake.
Aliongeza kuwa uchumi wa Zanzibar umeweza
kuimarika kwa kiasi kikubwa kutokana na kukua kwa sekta hiyo ya utalii hapa
nchini hatua ambayo imepelekea kuimarika kwa huduma mbali mbali za kimaendeleo
na kijamii huku ikiendelea kuwa kivutio duniani.
“Nuru ya Zanzibar inaendelea kungara na maendeleo
yanazidi kuimarika siku hadi siku…hongera sana kwa hatua ya kiuchumi
iliyofikiwa hapa Zanzibar, pongezi hizi nazitoa kwa dhati ya moyo wangu kabisa”,
alisisitiza Profesa Ndulu.
Aidha, Profesa Ndulu alimueleza Dk. Shein kuwa
kuimarika kwa uchumi wa Zanzibar hivi sasa kunatokana na uongozi imara wa Rais Dk.
Shein pamoja na utaalamu na uzoefu wake mkubwa wa uongozi alionao kwa muda
mrefu.
Pamoja na hayo, Profesa Ndulu alitumia fursa hiyo
kumueleza Dk. Shein mashirikiano mazuri yaliopo kati ya uongozi wa Wizara ya
Fedha Zanzibar na Benki hiyo hatua ambayo imeweza kuleta mafanikio makubwa
ndani ya uongozi wa miaka kumi akiwa Gavana wa BOT na matarajio aliyonayo ya
kuendeleza zaidi mafanikio hayo miaka kwa ijayo.
Sambamba na hayo, Profesa Ndulu alimueleza Dk.
Shein majukumu yake mengine atakayoyafanya katika masuala mazima ya kiuchumi na
kifedha kitaifa na kimataifa mara baada ya kumaliza muda wake wa kazi ya Gavana
wa (BOT).
Nae Rais Dk. Shein kwa upande wake alimpongeza
Gavana wa Benki ya Tanzania (BOT) anaemaliza muda wake Profesa Benno Ndulu
kutokana na mchango wake mkubwa alioutoa katika kuiimarisha na kuiendeleza
sambamba na kusimamia fedha za Tanzania katika Benki hiyo.
Dk. Shein alitumia fursa hiyo kumpongeza Profesa
Ndulu kwa kufanya kazi kwa mashirikiano makubwa kati yake na uongozi wa Wizara
ya Fedha wa Zanzibar sambamba na michango yake katika kuimarisha kada ya fedha
hapa nchini.
Katika mazungumzo hayo, Dk. Shein alieleza
kufurahishwa na maelezo ya Profesa Ndulu kuhusiana na kuimarika kwa uchumi wa
Zanzibar ambapo alisisitiza kuwa juhudi zake zimeweza kuendeleza juhudi za
kuimarisha uchumi kwa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar na Serikali ya Jamhuri
ya Muungano wa Tanzania.
Pamoja na hayo, Dk. Shein alieleza kuwa (BOT), ni
Benki ya Muungano ambayo imekuwa ikifanya vyema shughuli zake kwa pande zote
mbili za Jamhuri ya Muungano wa Tanzani.
Aidha, Dk. Shein Shein alieleza kuwa ipo haja ya
kujivunia mafanikio hayo makubwa ya kiuchumi yaliofikiwa hapa Zanzibar huku
akieleza matumaini yake ya kuendelea Benki hiyo kufanya vizuri chini ya uongozi
mpya wa Profesa Florens Luoga.
Rais Dk. Shein alimueleza Gavana huyo anaemaliza
muda wake kuwa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar chini ya uongozi wake
itaendelea kutoa ushirikiano mkubwa na Benki hiyo kupitia Tawi lake lililopo
Zanzibar.
Rajab Mkasaba, Ikulu
Zanzibar
Postal Address:
2422 Tel.:0777427449. Fax: 024 2231822
E-mail: rajabmkasaba@yahoo.co.uk
No comments:
Post a Comment