Habari za Punde

MKUTANO WA BARAZA LA VYUO VIKUU KATIKA NCHI ZA EAC WAWEKA MIKAKATI KUINUA ELIMU YA JUU



Viongozi na wajumbe wa mkutano Baraza la Vyuo Vikuu katika nchi za Afrika Mashariki(IUCEA) wakiimba wimbo wa Jumuiya ya Afrika Mashariki(EAC) wakati wa mkutano wa siku mbili uliofanyika jijini Nairobi Nchini Kenya ambao ulikweka mikakati ya kuimarisha viwango vya wahitimu ili kuweza kushindana katika soko la ajira.

Katibu Mtendaji wa Baraza la Vyuo Vikuu katika nchi za Afrika Mashariki(IUCEA),Profesa Alexander Lyambabaje akizungumza kwenye mkutano huo .

Baadhi ya Wakuu wa taasisi za elimu kutoka Tanzania ambao walikua sehemu ya mkutano huo,kushoto ni Makamu Mkuu wa Chuo cha Sayansi na Teknolijia cha Nelson Mandela mkoa wa Arusha,Profesa Kalori Njau na Mkuu wa Chuo cha Ushirika Moshi mkoa wa Kilimanjaro,Profesa Faustin Bee.

Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki wa Kenya na Maendeleo ya Ukanda wa Kaskazini,Peter Munya akimkabidhi Cheti mmoja wa wanafunzi waliofanya vizuri katika ubunifu ,kulia ni Katibu Mtendaji wa Baraza la Vyuo Vikuu katika nchi za Afrika Mashariki(IUCEA),Profesa Alexander Lyambabaje

Makamu Mkuu wa Chuo cha Sayansi na Teknolijia cha Nelson Mandela mkoa wa Arusha,Profesa Kalori Njau (kushoto) akitoa maelezo ya shughuli za kitaaluma katika Chuo chake kwa Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki wa Kenya na Maendeleo ya Ukanda wa Kaskazini,Peter Munya(katikati) ,Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki wa Uganda,Dk Kirunda Kivejinja na  viongozi wengine.


Katibu Mtendaji wa Tume ya Elimu ya Juu nchini (TCU),Profesa Charles Kihampa(katikati) akizungumza kwenye mkutano na waandishi wa habari kuhusu miakakti ya pamoja ya kuimarisha elimu ya juu katika nchi za Afrika Mashariki(EAC),kushoto ni Katibu Mtendaji wa Baraza la Vyuo Vikuu katika nchi za Afrika Mashariki(IUCEA),Profesa Alexander Lyambabaje na kulia ni Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha St Jonnes mjini Dodoma,Profesa Emmanuel Mbennah.

Washiriki wakiwa katika picha ya pamoja baada ya ufunguzi wa mkutano ulifanyika jijini Nairobi nchini Kenya.

Imeandaliwa na www.rweyemamuinfo.blogspot.com

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.