Habari za Punde

Omar King Afanya Ziara Kutembelea Mradi wa Ujenzi wa Uwanja wa Kisasa wa Mao Zedong leo.


Katibu Mkuu Wizara ya Vijana Utamaduni Sanaa na Michezo Zanzibar Omar Hassan Omar King, akiwa na Wajenzi wa Uwanja wa Kisasa wa Mao Zedong Zanzibar, akiwa na wasimamizi wa ujenzi huo kutoka China .Ligen Zhang na Yang Pan, wakiwa katika eneo la uwanja wa mpira ukiwa katika hatua ya uwekeji wa nyasi bandia mmoja ya viwanja hivyo.

Akizungumza na waandishi wa habari alipofanya ziara kutembelea Uwanja huo kuona maendeleo ya ujenzi wake hatua iliofikia na kusema Serikali ya Mapinduzi Zanzibar itaendelea kuimarisha Miundombinu ya viwanja vya michezo na kubadilisha mifumo ndani ya Sekta za michezo Zanzibar. ili kuona sekta hiyo inapiga hatua zaidi kuinua viwango vya michezo mbalimbali ilioko katika Visiwa vya Unguja na Pemba ili kusonga mbele zaidi kimataifa.

Katibu Mkuu ameyasema hayo wakati alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari za michezo Zanzibar mara baada ya kufanya ziara yake kutembelea mradi huo. Unaojengwa kwa ufadhili wa Serikali ya Watu wa Jamuhuri ya China na Serikali ya Mapinduzi Zanzibar.

Amesema mbali na juhudi zinazoendelea kuchukuliwa na Serikali ya Mapinduzi Zanzibar kuimarisha miundombinu katika sekta ya michezo ikiwemo ujenzi wa viwanja vya kisasa katika sehemu mbalimbali za visiwa vya Unguja na Pemba katika hatua za ujenzi wa viwanja vya kisasa vya michezo vya Wilaya.

Pia amesema itahakikisha kunakuweko na marekebisho ya mifumo ya Vyama vya michezo kuwa na viongozi wenye sifa za kuongoza sekta hiyo ya michezo 

Amesema maendeleo ya michezo Zanzibar yamekuwa yakipata vipingamizi kutokana na mfumo uliokuwepo katika tasnia ya michezo haiendani na mifumo ya maendeleo ya michezo duniani. 

Msimamizi wa Mradi huo wa Ujenzi wa Viwanja vya Kisasa vya michezo katika uwanja wa Mao Zedong  kutoka China Ligen Zhang pamoja na Meneja wake Yang Pan, amesema maendeleo ya ujenzi huo yanaendelea vizuri na matumaini yao ujenzi huo utakwenda kama ilivyopangwa kumalizika ujenzi wake kwa wakati uliopangwa. ili kutowa huduma za kimichezo kwa wananchi wa zanzibar.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.