Habari za Punde

Wabunge wa Zanzibar wapata ajali ya gari Morogoro

 Gari la Land Cruiser Prado lililopata ajali Mororgoro ambapo Wabunge sita kutoka Zanaibhra walijeruhiwa hivi leo usiku
Mmoja wa Wabunge kutoka Zanzibar akiwa amelazwa katika Hospitali ya Morogoro kwa ajili ya Matibabu


Wabunge sita kutoka Zanzibar wamepata ajali mbaya ya gari waka gari waliokuwa wakisafiria aina ya Land Cruiser Prado lilliokuwa likiendeshwa na mbunge wa Mfenesini kupinduka eneo la Morogoro.

Ajali hii ilitokea majira ya usiku wakati wabunge hawa wakiwa safarini.

Wabunge waliokuwemo katika gari lililopinduka ni Haji Ameir Haji (Makunduchi), Khamis Ali Vuai (Mkwajuni), Bhagwanji Maganlal Meisuria (Chwaka), Makame Mashaka Foum (Kijini), Juma Othman Hija (Tumbatu) wako hospitali kwa matibabu.

Mbunge wa Makunduchi Haji Ameir Haji inasemekana ndie aliejeruhiwa vibaya kwani alikuwa hakufunga mkanda.


Mganga mfawidhi hospitali ya rufaa Mkoa wa Morogoro, Dk Rita Lyamuya amesema majeruhi hao walipokelewa saa 3 usiku na kupatiwa huduma za awali.

"Jana tumepokea majeruhi sita walioumia sehemu mbalimbali na mmoja wao alilazimika kulazwa chumba cha wagonjwa wanaohitaji uangalizi wa karibu (ICU) lakini hali yake inaendelea vizuri,” amesema.

“Leo asubuhi tayari tumewapa rufaa kwenda hospitali ya Taifa Muhimbili kwa uchunguzi zaidi  zaidi.”No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.