Habari za Punde

Balozi Seif Azindua Visima vya Maji Vilivyojengwa na Taasisi ya ZARDEF.

 
Mwakilishi wa Jimbo la Mahonda Balozi Seif Ali Iddi akigawa Vifaa vya Michezo kwa Timu mbali mbali zilizomo ndani ya Jimbo lake hapo katika Ukumbi wa Mikutano wa CCM Jimbo hilo uliopo Kinduni.
Mwakilishi wa Jimbo la Mahonda Balozi Seif Ali Iddi akigawa Vifaa vya Michezo kwa Timu mbali mbali zilizomo ndani ya Jimbo lake hapo katika Ukumbi wa Mikutano wa CCM Jimbo hilo uliopo Kinduni. 


Na.Othman Khamis OMPR.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi ameinasihi Jamii kuepuka kukamiti ovyo na badala yake irejee katika Utamaduni ya Kuotesha Miti katika maeneo wanayoishi ili Ardhi iendelee kubakia katika maumbile yake ya kawadia.
Alisema hivi sasa kiwango cha maji katika Ardhi kinaendelea kupungua kutokana na tabia ya Wanaadamu kuchafua mazingira ikiwemo ukataji ovyo wa Misitu jambo ambalo ni hatari kwa maisha ya viumbe.
Balozi Seif Ali Iddi ambae opia ni Mwakilishi wa Jimbo la Mahonda alitoa nasaha hizo wakati wa sherehe za Uzinduzi wa Visima Viwili vya Maji safi na Salama vilivyochimbwa katika Kituo cha Afya Jimbo la Donge na Skuli ya Mshingi na Sekondari za Mahonda Jimbo la Mahonda.
Visima hivyo ikiwa miongoni mwa Visima 15 vitakavyochimbwa ndani ya Wilaya ya Kaskazini “B” ambapo Jimbo la Mahonda pekee vitakuwa Visima Vitano ni msaada kutoka Taasisi ya Kiraia ya Zanzibar Relief  and Development Foundation {ZARDEF} chini ya Ufadhili wa Ubalozi wa Uturuki Nchini Tanzania.
Balozi Seif alisema shida ya huduma za Maji safi na salama katika baadhi ya Maeneo Visiwani Zanzibar licha ya kusababisha na Ongezeko la Idadi ya Watu Nchini lakini bado pia  huchangiwa na uharibifu wa mazingira unaopaswa kuepukwa kwa nguvu zote.
Alisema akiwa msimamizi wa Shughuli za Serikali atafanya ziara katika maeneo mbali mbali kuangalia shughuli za Mazingira hasa kwa vile Taasisi hizo zimeingizwa katika Wizara yake kutokana na mabadiliko yaliyofanywa na Rais wa Zanzibar hivi karibuni katika Taasisi nza Umma.
Balozi Seif  aliwakumbusha Wananchi kwamba ni wajibu wa Walimu, Wanafunzi na Wananchi wote wa Majimbo la Mahonda na Donge kusimamia utunzaji wa Visiwa hivyo pamoja na rasilmali zilizomo katika Majengo ya huduma za Kijamii kama Skuli na Vituo vya Afya.
Alifahamisha kwamba Visima vilivyochimbwa ni waji wa wahusika hao kuhakikisha vinaendelea kudumu kwa muda mrefu kwa vile hauna asiyetambua kwamba Maji ni neema kwa Wanaadamu pamoja na Viumbe vyote vyenye Uhai.
Alisema haitakuwa ni jambo la busara kwa Viongozi pamoja na Taasisi zinazofadhili Miradi ya Jamii katika maeneo tofauti Nchini kupata Taarifa ya uwepo wa uharibifu wa Miradi wanayofadhili.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar  aliiahidi Taasisi ya Kiraia ya Zanzibar Relief and Development Foundation {ZARDEF}kuipa kila msaada katika kuona Malengo iliyojipangia inayatekeleza kwa ufanisi mkubwa.
Balozi Seif alisema Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar inathamini jitihada na Malengo iliyojiwekea Taasisi hiyo inayokwenda sambamba na Serikali katika kuimarisha Miradi ya Maendeleo kwa Wananchi wote hasa katika Sekta za Kilimo, Uvuvi na Biashara.
Akitoa Taarifa ya Miradi ya Uchimbaji wa Visima katika maeneo mbali mbali Nchini Mratibu wa Taasisi ya ZARDEF Bwana  Salum Ramadhan Abdulla alisema Taasisi hiyo kwa sasa imejikita katika uchimaji wa Visima vya Maji ikidhamiria  kusaidia kuondoa tatizo la Huduma hiyo  ifikapo Mwaka 2020.
Bwana Salum alisema utafiti umeonyesha wazi kwamba kundi kubwa linaloendelea kuathirika na ukosefu wa huduma ya Maji safi na salama ni Wanawake na Watoto wanaolazimika wakati mwengine kuacha shughuli zao za kujitafutia riziki na Masomo.
Mratibu huyoi wa ZARDEF aliongeza kwamba Taasisi hiyo imejiwekea malengo ya muda mrefu katika kuimarisha Miradi Minne Mikubwa itakayoelekezwa zaidi kwa kundi kubwa la Vijana katika azma ya kuwaondoshea changamoto ya upatikanaji wa ajira.
Aliitaja Miradi hiyo kuwa ni pamoja na Mafunzo ya Uzasiriamali, Uvuvi wa Samaki utakaohusisha Boti Tatu  kubwa zitakazolenga uvuvi wa bahari kuu, Kilimo cha Kisasa pamoja na ufugaji wa kuku na Ng’ombe wa Kisasa.
Mratibu huyo wa ZARDEF aliiomba Serikali Kuu kutoa agizo Maalum la kuja kuyataka  Mahoteli ya Kitalii Nchini kununua bidhaa za Samaki  pamoja na zile za Mboga Mboga zitakazotokana na Mradi huo.
Akitoa shukrani kwa Niaba ya Wananchi wa Majimbo ya Mahonda na Donge Mwakilishi wa Jimbo la Donge ambae pia ni Waziri wa Fedha na Mipango Zanzibar Dr. Ghalid Salum Mohamed ameipongeza Taasisi ya Kiraia ya ZARDEF kwa uharaka wa malengo yake iliyojipangia.
Dr. Khalid alisema Visima hivyo viwili vilivyochimbwa ndani ya maeneo ya Makundi ya Jamii katika huduma za Kitabibu na Elimu ni sadaka Maalum ya Wananchi Wawili wa Uturuki ambapo Mmoja ni Marehemu wenye Mapenzi na Zanzibar.
Aliihakikishia Taasisi ya ZARDEF kwamba Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar itaendelea kushirikiana na Taasisi hiyo na pale itapobidi itakuwa tayari kusamehe Kodi kwa baadhi ya Vifaa vitakavyoletwa Nchini kwa kusaidia huduma mbali mbali za Kijamii.
Akitoa salamu zake Balozi wa Uturuki Nchini Tanzania Bwana Ali Davutoglu alisema visima hivyo viwili vilivyozinduliwa ni alama ya ushirikiano kati ya Uturuki na Zanzibar na Tanzania kwa ujumla.
Alisema Ubalozi wa Uturuki Nchini utajitahidi katika kuona ushirikiano huo unazidi kuimarika na kudumu kwa muda mrefu ambapo alisisitiza kwamba Uongozi wa Ubalozi huo uko tayari kusaidia Miradi ya huduma za Umeme pale itapoonekana yapo mahitaji katika sekta hiyo mahali popote Nchini Tanzania.
Visima viwili vilivyochimbwa katika Kituo cha Afya cha Donge Kitaluni na Skuli ya Mahonda Msingi na Sekondari na kusimamiwa na Taasisi ya ZARDEF chini ya Ubalozi wa Uturuki Nchini Tanzania vina thamani ya shilingi Milioni 11,300,000/- ambapo kila kimoja gharama yake ni shilingi Milioni 5,650,000/-.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.