Kamishna wa Operesheni wa Jeshi
la Zimamoto na Uokoaji, (CF) Billy Mwakatage, akipokelewa na Maafisa wa Jeshi
hilo pamoja na mwenyeji wake ambaye ni mmiliki wa Yatch Club Bw. Brian
Fernandes, alipokwenda kufunga mafunzo ya uzamiaji majini kina kirefu daraja la
pili kwa Askari wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji. Mafunzo hayo yalikuwa
yakifanyika katika kisiwa cha Bongoyo kilichopo ndani ya bahari ya hindi, Jijini
Dar es Salaam.
Mzamiaji wa kikosi maalum
cha Uokoaji majini wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, Sajini Gift Longwe,
akionesha mbinu mbalimbali za uzamiaji majini kwenye kina kirefu walizojifunza
toka kwa wakufunzi kutoka nchini Ujerumani, kwa mgeni rasmi Kamishna wa Operesheni wa
Jeshi hilo, (CF) Billy Mwakatage (hayupo pichani). Wakati wa hafla ya kufunga
mafunzo ya uzamiaji majini kina kirefu daraja la pili kwa Askari wa Jeshi la
Zimamoto na Uokoaji, mapema leo Jijini Dar es Salaam.
Kamishna wa Operesheni wa Jeshi
la Zimamoto na Uokoaji, (CF) Billy Mwakatage (katikati), akimkabidhi cheti
mmoja ya wahitimu wa mafunzo ya uzamiaji majini kina kirefu, Sajini Gift Longwe
(kushoto). Wakati wa hafla ya kufunga mafunzo ya uzamiaji majini kina kirefu
daraja la pili kwa Askari wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, mapema leo Jijini
Dar es Salaam.
Wazamiaji wa kikosi maalum
cha Uokoaji majini wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, Sajini Gift Longwe
(kushoto) na Koplo Siwizan Kazimoto (kulia), wakionesha umahili wao wa uzamiaji
majini kwenye kina kirefu mbele ya mgeni Kamishna wa Operesheni wa Jeshi hilo,
(CF) Billy Mwakatage (hayupo pichani). Wakati wa hafla ya kufunga mafunzo ya
uzamiaji majini kina kirefu daraja la pili kwa Askari wa Jeshi la Zimamoto na
Uokoaji, mapema leo Jijini Dar es Salaam. (Picha na Jeshi la Zimamoto
Na Uokoaji)
No comments:
Post a Comment