Waziri wa Habari
Utamaduni Sanaa na Michezo Dkt.Harrison Mwakyembe (watatu kushoto) akimkabidhi
bendera msanii wa filamu nchini Yvonne Cherrie maarufu kama Monalisa jana
jijini Dar es Salaam anayetarajia kwenda nchini Ghana mapema wiki hii katika
tuzo za The African Prestigious Awards ambapo amechaguliwa kuwania kipengele
cha Msanii Bora wa Kike Afrika,wa pili
kulia ni Kaimu Mkurugenzi Idara ya
Maendeleo ya Sanaa Bibi. Leah Kihimbi na wa kwanza kushoto ni Katibu Mtendaji
Bodi ya Filamu Tanzania Bibi. Joyce Fissoo.
Waziri wa Habari
Utamaduni Sanaa na Michezo Dkt.Harrison Mwakyembe (wapili kushoto) akimkabidhi
Msanii wa Filamu nchini Yvonne Cherrie maarufu kama Monalisa tiketi ya ndege jana jijini Dar es Salaam kwa
ajili ya safari yake ya kwenda nchini
Ghana mapema wiki hii katika tuzo za The African Prestigious Awards
ambapo amechaguliwa kuwania kipengele cha Msanii Bora wa Kike Afrika,kutoka
kulia wapili ni Kaimu Mkurugenzi Idara ya Maendeleo ya
Sanaa Bibi. Leah Kihimbi na wa kwanza kulia ni Katibu Mtendaji Baraza la Sanaa
Tanzania Bw.Godfrey Mngereza.
Katibu Mtendaji Bodi
ya Filamu Tanzania Bibi. Joyce Fissoo(wakwanza kushoto) akifafanua kwa
waandishi wa habari na wadau wa sanaa (hawapo pichani) kuhusu tuzo za The
Africa Prestigious Awards jana jijini Dar es Salaam zitakazotolewa nchini Ghana
hivi karibuni kwa kueleza heshima ya
tuzo hizo na Tanzania imepata heshima ya Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano
wa Tanzania Dkt.John Pombe Magufuli nae kuteuliwa kuwania tuzo ya kiongozi bora
Afrika,wa kwanza kulia ni Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo
Dkt.Harrison Mwakyembe.
Msanii wa Filamu
nchini Yvonne Cherrie maarufu kama
Monalisa akiahidi kwa Waziri wa habari
Utamaduni Sanaa na Michezo Dkt.Harrison Mwakyembe (hayupo pichani) jana jijini Dar es Salaam katika sherehe ya
kukabidhiwa bendera kuwa atarudi na tuzo
hata kama yeye hatopata basi ataweza na kurudi na hata tuzo ya Msanii Raymond Kigosi
anayewania Tuzo ya Msanii Bora wa Kiume Afrika au Tuzo ya Msanii King Majuto
anayewania Tuzo ya Mchekeshaji Bora Afrika au Mpiga picha Moiz Hussein anayewania
Tuzo ya Mpiga picha Bora Afrika katika tuzo za The African Prestigious Awards
zitakazotolewa nchini Ghana hivi
karibuni,wa kwanza kulia ni Mama Mzazi wa Msanii Monalisa Bibi Suzan Lewis
maarufu kama Natasha.
Na Anitha Jonas –
WHUSM.Dar es Salaam.
Utendaji uliyotukuka
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.John Pombe Magufuli na ukuwaji wa sekta ya filamu nchini ndiyo
vinavochangia kuitangaza nchi yetu katika tuzo za The African Prestious Awards.
Kauli hiyo imetolewa
jana jijini Dar es Salaam na Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo
Mhe.Dkt.Harrison Mwakyembe alipokuwa akimkabidhi bendera msanii wa filamu
nchini Yvonne Cherrie Maarufu kama Monalisa anayetarajia kwenda nchini Ghana
katika tuzo hizo.
“Tanzania imepata
heshima kubwa katika tuzo hizi zenye heshima kubwa katika bara la Afrika ambapo
Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.John Pombe Magufuli
ameteuliwa kuwania Tuzo ya Kiongozi Bora Afrika, napia tuna wasanii watatu
ndani ya tansia ya filamu ambao ni King Majuto anayewania Tuzo ya Mchekeshaji Bora
Afrika,Raymond Kigosi anayewania Tuzo ya Msanii Bora wa Kiume Afrika na
Monalisa mwenyewe anayewania Tuzo ya Msanii Bora wa Kike Afrika pamoja na Mpiga
picha Mahiri
Moiz Hussein anayewania Tuzo ya Mpiga Picha Bora Afrika,”alisema
Dkt.Mwakyembe.
Akiendelea kuzungumza
katika sherehe hiyo ya kukabidhi bendera Mheshimiwa Mwakyembe aliwasisitiza
wasanii wanchini kuendelea kuandaa kazi zinazoonyesha ubunifu wao kwani ukuaji
wa tansia ya filamu Tanzania uko mikononi mwao na si vinginevyo.
Pamoja na hayo nae Msanii
wa Filamu nchini Yvonne Cherrie Maarufu kama Monalisa anayetarajia kuondoka
nchini mapema wiki hii kwenda nchini Ghana kwa ajili ya Tuzo hizo aliwaahidi watanzania kuwa lazima atarudi na tuzo
kwani anawawakilisha wasanii wenzake hao wawili pamoja na mpiga picha huyo
aliyetajwa na pia aliishukuru serikali kwa kumpatia tiketi kwa ajili ya
kufanikisha safari hiyo.
“Tuzo hizi
nazichukulia kama ni heshima kubwa sana kwangu kwani kipengele ninachowania
kinahusisha wasanii wakubwa katika bara la afrika kwani niko pamoja na Lupita Nyongo ambaye ni
mwigizaji wa Hollywood pamoja na Jackie Apia ambaye nae anafanya vizuri hivyo
hata nisipopata tuzo hii kwangu kuchaguliwa kwanza katika kipengele hicho
tayari ni ushindi kulinga na uwezo wasanii wenzangu tuona shindana,”alisema
Monalisa.
Kwa upande wa Katibu
Mtendaji Bodi ya Filamu nchini Bibi.Joyce Fissoo alisema anafurahishwa kuona
sekta ya filamu ya nchini ikikua na kuleta taswira mpya katika bara la afrika
ambapo wasanii watanzania nao kazi zao zinavuka mipaka na kuleta changamoto
katika ushindani katika tasnia filamu Afrika.
Hata hivyo nae mama
mzazi wa Monalisa Bibi.Suzan Lewis maarufu kama Natasha alieleza kufurahishwa
na kazi ya filamu anayoifanya mwanaye na pia alieleza kuwa anamtakia mafanikio
makubwa pamoja na kushinda tuzo hiyo.
No comments:
Post a Comment