Habari za Punde

Mashabiki wa Chelsea walikuwa wazuri sana - Mourinho

Mourinho alipoulizwa kuhusu heshima kati yake na mashabiki wa Chelsea, alisema: "Kitu pekee ninaweza kusema kuhusu mashabiki wa Chelsea ni kwmaba tangu siku yangu ya kwanza 2004 hadi siku ya mwisho nilipofutwa miaka kadha iliyopita, waliniunga mkono kikamilifu," alisema Mourinho, 55, aliyeshinda vikombe vinane akiwa Stamford Bridge.
"Waliniunga mkono kila siku. Waliniunga mkono kila mechi, waliniunga mkono haa siku nilipofutwa - mara mbili, moja 2008 na miaka kadha iliyopita.
"Hilo sitalisahau kamwe kwa sababu walifanya kile ambacho ninaamini mashabiki wazuri hufanya, ambacho ni kumuunga mkono meneja wao hadi siku ya mwisho.
"Kuhusu mashabiki wa Chelsea, hilo sisahau: walikuwa wazuri sana."
Mourinho ndiye meneja aliyefanikiwa zaidi Chelsea baada ya kushinda mataji matatu vipindi viwili alivyokuwa Stamford Bridge mwaka 2005, 2006 na 2015.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.