Habari za Punde

Matukio ya Picha Mtaa kwa Mtaa Zenj leo.

Wachuuzi wa Samaki katika Marikiti Kuu ya Darajani Unguja wakiwa katika Mnada wa Samaki wa aina mbalimbali waliowasilishwa katika mnada huo na Wavuvi kutoka sehemu mbalimbali, katika mnada huo samaki aina ya nguru ameuzwa kwa shilingi 50,000/=  inategemea hali ya mnada leo asubuhi na wingi wa bidhaa hiyo katika mnara huo. 

Baadhi ya Samaki wa aina mbalimbali wakiwa katika kibaraza la mnada wakisubiri kunadishwa na Dalali. 
Ndizi za aina ya mkono mmoja zikiwa katika marikiti kuu ya darajani Zanzibar mkungu mmoja uliuzwa kati ya shilingi 25,000/= inategemea ukubwa wake na ndizi moja iliuzwa kati ya shs.2000/= na 3500/= kwa ndole moja na Ndizi aina ya mtwike iliuzwa chana moja shilingi 4500/=  

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.