




Na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii,Kanda ya Kaskazini .
serikali mkoani
Kilimanjaro imezindua kamati ya Maafa ya mkoa ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa
Sheria namba 7 ya mwaka 2015 kwa lengo la kumshauri Mkuu wa mkoa kuhusu masuala
ya usimamizi wa maafa na kuratibu shughuli za dharura miongoni mwa taasisi za
kisekta za serikali za mitaa.
Mbali na majukumu
hayo kamati hiyo pia itakuwa na wajibu wa kutafuta rasilimali kwa ajili ya
usimamizi wa maafa katika mkoa,kufungamanisha mfumo wa tahadhari ya awali
katika mkoa na kuwezesha uanzishaji wa mfumo wa takwimu na taarifa za maafa za
mkoa kwa kushirikiana na wakala.
Akizindua kamati
hiyo inayoundwa na wajumbe kutoka taasisi mbalimbali zikiwemo za
kidini,wafanyabiashara ,Wataalamu mbalimbali pamoja na wajumbe wa kamati ya
ulinzi na usalma ya mkoa ,Mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro ,Anna Mghwira alisema kwa
kipindi kirefu mkoa haujawa na kamati ya maafa iliyo hai ,inayojitambua na
kuwajibika ipasavyo.
“Sheria hii
inatafsriri maafa kwamba ni ya kimkoa kama zaidi ya wilaya moja ndani ya mkoa
imeathirika au kama wilaya,mji au manispaa husika haina uwezo wa kushughulikia
tatizo hilo au kama tatizo hilolimehusisha wilaya zinazopakana ndani ya mkoa
“alisema Mghwira.
Mghwira alitoa
maelekzo kwa wakuu wa wilaya kuhakikisha kamati za maafa za wilaya ,kata na
vijiji zinaundwa na kusimamiwa ili zitekeleze majukumu yake ipasavyo kwa mujibu
wa sheria hiyo huku akiwaagiza wakulurugenzi kuwawezesha wakuu wa wilaya
kuandaa utaratibu wa kutoa maelekezo kwa kamati a wilaya ,kata na vijiji .
“Hakuna haja ya
kusubiri maafa yatokee ndiyo tufanye maandalizi ,tuanze sasa,kwa taarifa
nilizonazo mvua bado zinaendelea ,twendeni katika maeneo yanayotuzunguka kutoa
tahadhari za awali kwa wananchi wote wanaooonekana kupata madhara kutokana na
mvua zinazoendelea kunyesha”alisema Mghwira.
Mwisho.
No comments:
Post a Comment