Habari za Punde

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi Azindua Mfumo wa Kisasa wa Mawasiliani Vedio Confrence.

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif  Kulia akishiriki  moja kwa moja kutokea Zanzibar  tukio la Uzinduzi wa mfumo wa Kisasa wa Mawasiliano {Vedio Conference} wa Kampuni ya Simu Tanzania {TTLC} uliofanyika Mjini Dar es salaam ambapo Mgeni rasmi alikuwa Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dr. John Pombe Magufuli.
 Balozi Seif Ali Iddi Kushoto akizungumza moja kwa moja kutokea Zanzibar  kwenye Uzinduzi wa mfumo wa Kisasa wa Mawasiliano {Vedio Conference} wa Kampuni ya Simu Tanzania {TTLC} uliofanyika Mjini Dar es salaam.
Meneja wa Kampuni ya Simu Tanzania {TTCL} Kanda ya Zanzibar Bwana Mohamed Yussuf  Mohamed akiishukuru SMZ kwa kuiunga mkono katika maandalizi ya kuanza kwa mfumo wa mawasiliano ya Kisasa ujuilikanao Vedio Conference mara baada ya kumaliza hafla hiyo fupi. Picha na – OMPR – ZNZ.
Na.Othman Khamis OMPR.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi alisema wakati umefika kwa Taasisi za Umma, Binafsi na hata Wananchi wa Kawaida Nchini kurejesha matumaini yao katika kupata huduma za mawasiliano kupitia Kampuni ya Simu Tanzania {TTLC } kutokana na maboresho makubwa ya kisasa yaliyofanywa ndani ya Kampuni hiyo.
Balozi Seif Ali Iddia alitoa kauli hiyo mara baada ya kumalizika kwa uzinduzi mfumo wa Kisasa wa Mawasiliano {Vedio Conference} wa Kampuni ya Simu Tanzania {TTLC} ambapo Mgeni rasmi alikuwa Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dr. John Pombe Magufuli.
Uzinduzi huo umefanyika Jijini Dar es salaam ambapo Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akiwa Zanzibar na Waziri Mkuu Mh. Kassim Majaliwa Kassim akiwa Mjini Dodoma waliunganishwa moja kwa moja kwenye uzinduzi huo.
Balozi Seif alisema kazi kubwa iliyofanywa na Kampuni ya Simu Tanzania kwa sasa imeanza kuleta matumaini makubwa kwa Umma katika upatikanaji wa huduma za Mawasiliano tofauti ya kipindi cha nyuma ambacho huduma hizo zilizkuwa zikipatikana kwa mgao.
Balozi Seif alisema kufuatia mfumo huo mpya wa Mawasiliano kwa njia ya Vielelezo vya Picha {Vedio Conference }, kwa sasa hana haja ya kumfuata  Rais wa Jamuhuri, makamu wa Rais wa Jamuhuri au Waziri Mkuu upande wa Tanzania Bara kwa mambo ya dharura yanayowajibika kutekelezwa katika kipindi kifupi.
Mapema Meneja wa Kampuni ya Simu Tanzania {TTCL} Kanda ya Zanzibar Bwana Mohamed Yussuf Mohamed alimueleza Balozi Seif  kwamba TTCL hivi sasa inakamilisha ufungaji wa baadhi ya vifaa vitakavyowawezesha  Viongozi Wakuu kuzungumza kwa pamoja wakiwa maeneo mbali mbali.
Bwana Mohamed alisema hatua hiyo mbali ya kupunguza gharama lakini pia imezingatia kwenda sambamba na mfumo wa Teknolojia ya Kisasa inaendelea kuendena katika Mataifa m,bali mbali Duniani.
Meneja huyo wa TTLC Zanzibar aliishukuru Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kwa kuiunga mkono kwa asilimia kubwa iliyowezesha kufanikisha maandalizi ya Awali ya matumizi ya Mfumo huo mpya hapa Nchini.
Katika uzinduzi huo Uongozi wa Kampuni ya Simu Tanzania {TTCL} kupitia Mkurugenzi wake Mkuu Waziri Kindamba imetoa gawio la shilingi Bilioni 1.5 kutokana na faida ya shilingi Bilioni 28.5 baada ya kulipa Kodi.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.