Habari za Punde

Mhe Hassan Khamis Amewataka Wanafunzi Kidatu Cha Sita Kuwa Wazalenzo.

Na.Takdir.Ali,-Maelezo Zanzibar.  25-06-2018.
Naibu Waziri wa Wizara ya Biashara na Viwanda Mh.Hassan Khamis Hafidhi amewataka Wanafunzi wanaomaliza masomo ya kidato cha 6 kuwa Wazalendo na kuwa mstari wa mbele katika kujenga maendeleo ya nchi yao sio kukimbilia katika nchi za watu.
Amesema ni jambo la kusikitisha kuona kuwa Wazanzibar wengi wanaomaliza masomo hasa ya elimu ya juu wamekuwa wakikimbilia nje ya nchi na kupelekea kukosa wataalamu wakutosha na wenye uzalendo wa nchi yao.
Akizungumza katika Mahafali ya 3,Skuli ya Sekondari Faraja iliopo Kwa Mtipura amesema Uzalendo ni kitu cha msingi hivyo ni vyema kurudi katika nchi yao mara wanapomaliza masomo nje ya nchi ili kuja kutoa ujuzi walioupata kwa jamaa zao na Taifa kwa ujumla.
Amefafanua kuwa Serikali inategemea kupata wataalamu wazalendo watakaoweza kutumia utaalamu wao kwa katika masuala kama vile ya Gesi, Mafuta na kilimo cha umwagiliaji ili zanzibar iepukane na tatizo la umasikini lililodumu kwa muda mrefu.
Aidha amewataka wanafunzi hao wasisahau kuwa Serikali inatumia rasilimali nyingi kuwasomesha lakini kitendo cha kutorudi nyumbani kinapelekea kutofikia malengo ya Serikali ya kuwa na watalamu wakutosha katika nyanja mbali mbali za kijamii.
Amefafanua kuwa kila mwaka Zanzibar imekuwa ikipeleka wanafunzi masomea fani tofauti tofauti ilikemo Afya,Elimu, kilimo, mifugo,uvuvi, Habari na Mawasiliano ili kuweza kupata wataalamu wazalendo watakaoweza kuijenda nchi yao na kuepukana na kutegemea wataalamu kutoka nchi za nje.
Kinyume na hayo na hayo amesema mjenzi wa Zanzibar ni Mzanzibar mwenyewe hivyo endapo vijana wanaokwenda kusoma katika nchi za nje hawatakuwa wazalendo na kurejea katika nchi yao maendeleo yataendelea kubaki kuwa nyuma siku hadi siku.
Aidha Naibu huyo amewataka waalimu kuwasomesha wanafunzi somo la uzalendo ili kuweza kuwajenga kisaikolojia kwa kuipenda nchi yao na kuweza kuileta maendeleo.
Mbali na hayo amewataka wanafunzi hao wanapokuwa ndani au nje ya nchi kuchukuwa juhudi za kuhakikisha Zanzibar inaendelea kubaki katika hali ya Amani na Utulivu kwani ndio rasilimali kubwa ya nchi yetu.
Hata hivyo amewataka kuunga mkono juhudi zinazochukuliwa na serikali na sio kuwapaka matope kutokana na kasumba za kisiasa kwani wakati wa siasa umepita wasubiri mwaka 2020 kwa uchaguzi.
Kwa upande wake Ameir Khamis Bakari Mwalimu Mkuu skuli ya Faraja amesema tangu miaka mitatu wanafunzi wao walipoanza kufanya mitihani ya kidato cha sita wameweza kupasisha kwa asilimia mia moja jamboa ambalo linatokana na mashirikinaoa mazuri walionayo wazazi,waalimu na wanafunzi.
Sambamba na hayo amesema wamekuwa wakifanya juhudi za kila aina kuhakikisha wanafunzi wanaomaliza skuli wanakuwa raia wema wa kutumia kuijenga nchi yao.
               Imetolewa na Idara ya Habari Maelezo Zanzibar.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.