Habari za Punde

Mswada wa Sheria za Kutoza Kodi Wapitishwa Baraza la Wawakilishi Zanzibar

Na Miza Kona Maelezo Zanzibar.         27/06/2018.
Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Khalid Salum Mohamed amesema kupitishwa kwa Mswaada Sheria ya Kutoza Kodi itakuwa ni chachu ya kuimarika kwa ukusanyaji wa mapato nchini.
Hayo ameyasema huko katika Ukumbi wa Baraza la Wawakilishi Chukwani wakati akiwasilisha Mswaada wa Sheria za kutoza Kodi na Kubadilisha baadhi ya Sheria za Fedha na Kodi Kuhusiana na Ukusanyaji na Udhibiti wa Mapato ya Serikali na Mambo mengine kama hayo.
Amesema kuwa kuwepo kwa sheria hiyo kutasaida kuimarisha kwa ulinzi na kuzuia magendo na kupunguza miaya ya uingizaji wa biashara kwa njia hiyo ya magendo ambayo inakosesha pato la serikali na kukua kwa uchumi.
Amefahamisha kuwepo kwa udhibiti imara katika vyanzo vya mapato na kuweka mfumo bora wa kuzuia magendo kutaweza kuongeza ukusanyaji wa mapato na kuleta unafuu kwa walipa kodi.
Ameleeza kuwa sheria hiyo pia itaweza kupunguza miaya ya uingizaji wa biashara kwa njia ya magendo ambayo inakosesha pato la serikali na kukua kwa uchumi.
Akisoma Hotuba ya Kamati ya Bajeti ya Baraza la Baraza la Wawakilishi kuhusiana na maoni ya Mswaada huo Mjumbe wa Kamati hiyo Mhe. Shehe Hamad Mattar amesema kufanyiwa marekebisho ya sheria hiyo itawapa uwezo na nguvu zaidi maafisa wanaohusika na kuzuia magendo kwa kuwekwa mikakati imara ya kuweza kudhibiti.
Ameeleza kuwa sheria hiyo itaweza kudhibiti magendo ya aina zote na kuimarika ukusanyaji wa mapato ya serikali.
“Madhumuni ya mswaada huu ni kufanya mabadiliko katika baadhi ya sheria zinahusiana na ukusanyaki na udhibiti wa mapato ya serikali na mambo mengine yanayohusiana na hayo ili kuleta ufanisi zaidi katika utekelezaji wa sheria hizo”, alieleza Mjumbe huyo.
Aidha amesema miongoni mwa sheria zilizofanyiwa marekebisho na mswaada huo ni sheria ya kikosi maalum cha Kuzuia Magendo Nam. 1ya 2003 ili kukipa uwezo zaidi kikosi cha Kikosi Maalum cha Kuzuia Magendo katika kupambana na magendo ambayo yanachangia kupunguza ufanisi wa ukusanyaji wa mapato.
Aidha Mhe. Mattar afahamisha kuwa sheria ya kutoongeza kodi inapaswa kwenda sambamba na juhudi za usimamizi wa mapato kwa kupunguza miaya ya uvujaji wa mapato na kuwezesha kufikiwa malendo yaliyokadiriwa kutokana na vyanzo vya mapato vilivyopo.
Wakichangia mswaada huo Wajumbe wa Baraza hilo wamewaomba kufanyiwa uchunguzi wafanyabiasha ili kuepuka uingizaji wa biashara haramu pamoja na kuwataka kulipa kodi kwa lengo la kimarisha uchumi na kuongeza mapato nchini.
Wajumbe hao wameupisha mswaada huo wa Sheria  Sheria za kutoza Kodi na Kubadilisha baadhi ya Sheria za Fedha na Kodi Kuhusiana na Ukusanyaji na Udhibiti wa Mapato ya Serikali na Mambo mengine kama hayo.
MWISHO
IMETOLEWA IDARA YAHABARI MAELEZO ZANZIBAR.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.