Habari za Punde

Mtu wa Marree: Ni Nani Aliyemchora Mtu Huyu Mwenye Urefu wa Kilomita 4.2

Wiki hii inaadhimisha miaka 20 tangu rubani wa ndege aina ya helikopta aliyekuwa katika anga ya Australia kuona picha kubwa ya mtu aliyekuwa amechorwa katika ardhi.
Picha hiyo yenye urefu wa kilomita 4.2, kwa urefu katika eneo la juu la mlima lililopo tambarare kusini mwa Australia inaonekana kufanana na mwindaji wa jamii ya Aborigin.
Jina la mchoro huo la Marree Man linatokana na jina la kijiji kilichopo karibu ikiwa ni mojawapo ya michoro mikubwa kuwahi kuchorwa ardhini.
Lakini bado haijulikani ni nani aliyemchora mtu huyo-na kwa nini alifanya hivyo.Mapema wiki hii, mjasiriamali wa Australia Dick Smith alitoa dola $ 5,000 za Australia (£ 2,800; $ 3,700) ikiwa ni malipo ya taarifa yoyote kuhusu asili ya sanaa.
"Imehifadhiwaje kwa siri kwa miaka 20?" alisema katika Shirika la Utangazaji la Australia (ABC) Jumatatu.

'Ufanyikaji'

Marree Man imekuwa jambo la kujifurahisha tangu ugunduzi wake jangwani yapata kilomita 700 kaskazini mwa Adelaide. Imepata umaarufu kwenye ndege za utalii kwa sababu ni kubwa mno kutazamwa kutoka chini.
Ramani
Kwa kipimo cha jumla ya kilomita 28, Marree Man alikuwa na kina cha awali cha sentimita 35 (14 inchi), kwa mujibu wa ripoti za vyombo vya habari.
Wananchi wanaamini kuwa inaonyesha mtu wa aborigin akiwa amebeba woomera - fimbo ya kutupa - katika mkono wake wa kushoto. Phil Turner anaamini kuwa mchoraji , au wachoraji wake, walikuwa "wataalamu" ambao huenda walitumia teknolojia ya GPS.
"Yeyote aliyechora mstari huo aliweka alama ya skewers katika kila mita 10," bwana Turner aliiambia BBC. "Iwapo hukuweka vishirikishi vyovyote ingekuwa vigumu kujua iwapo umesimama katika kidole chake cha kulia ama katika kisukusuku chake.. Ukizingatia kwamba teknolojia ya GPS ilikuwa ndio imeanza kutumiwa wakati huo , ni ajabu juu ya ajabu."
Bwana Smith anakubaliana, akiwaambia ABC: "Hakukuwa na makosa - ilifanyika kitaaluma
Nadharia kadhaa kuhusu wachoraji wake zimeenea kwa miaka kadhaa sasa.
Kisiki kilichotumiwa kumchora Marree Man, kulingana na wakaazi.Haki miliki ya pichaPHIL TURNER
Image captionKisiki kilichotumiwa kumchora Marree Man, kulingana na wakaazi.
Rubani Trevor Wright, mtu wa kwanza kumgundua Maree Man mnamo tarehe 26 mwezi Juni 1998, anasema kuwa aliiona kwa bahati nzuri.
Hatahivyo ujumbe usiojulikana mwenyewe ulitumwa kwa wafanyiabishara wa eneo hilo na vyombo vya habari wakati huo kuwaeleza kuhusu uwepo wa Maree Man.
Baadhi ya watu wanashuku kwamba ni kazi ya wasanii wa Marekani kwa sababu ujumbe uliosambazwa ulitumia herufi za Marekani na kumbukumbu.
Lakini wengine wamesema kuwa ishara zilizotolewa sio za kweli, huku wengine wakisema kuwa mchoro huo ulifanywa na wakaazi wa eneo hilo na hasa wanachama wa jeshi la Australia.
Watu wa jamii ya Arabana ndio wamiliki wa eneo hilo ambalo Maree Man alichorwa. Meneja wa shirika la Arabana Aboriginal Lorraine Merrick alisema kuwa kuonekana kwa mchoro huo 1998 kuliwakasirisha wakaazi wa eneo hilo waliodai kwamba ulikuwa uharibifu wa ardhi yao.
Anasema kuwa kuna hisia tofauti kuhusu mchoro huo. Hatahivyo bi Merrick anasema kuwa shirika hilo linatambua kwamba Maree Man ni 'mtu tajika'.
Ni wazi sasa kwamba huwezi kurudisha nyuma wakati , aliambia BBC. HIvyobasi kwetu sisi ni kuufanyia mipango wa siku zijazo.
Marree Man ameonekana kufutika katika kipindi cha miaka kadhaa sasa lakini wakaazi kupitia ruhusa ya wakaazi wa jamii ya Arabana , wamekuwa wakitumia mashine waliimarisha mchoro huo 2016.
''Pengine kutojua mtu aliyechora picha hiyo ndio swala linalozidi kuvutia watu ,lakini hakuna watu wanaokuja kwangu kuniuliza ni nani aliyechora picha hiyo'' , alisema bi Merrick.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.