Habari za Punde

Waziri wa Biashara na Viwanda Zanzibar Amefanya Uteuzi wa Wajumbe wa Bodi ya Mamlaka ya Maendeleo ya Viwanda Vidogovidogo na Vya Kati Zanzibar (SMIDA)


Waziri wa Biashara na Viwanda Zanzibar Balozi Amina Salum Ali amefanya uteuzi wa wajumbe wa Bodi ya Mamlaka ya Maendeleo ya Viwanda Vidogo Vidogo na vya Kati (SMIDA).
Walioteuliwa ni Dkt. Abdalla Rashid Abdalla kutoka Wizara ya Biashara na Viwanda, Nd. Bakari Ali Silima Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali,  Nd. Ameir Haji Shehe kutoka Wizara ya Kazi, Uwezeshaji, Wazee, Wanawake na Watoto, Nd. Ahmed Yussuf kutoka Umoja wa Wazalishaji wadogo wadogo na Nd. Fatma Mbarouk Khamis kutoka Zanzibar.
Uteuzi huo unafuatia uteuzi wa Mwenyekiti wa Bodi ya Mamlaka ya Maendeleo ya Viwanda Vidogo Vidogo na vya Kati uliofanywa na Mheshimiwa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi hivi karibuni.
Waziri wa Biashara  na Viwanda amefanya uteuzi huo kwa mujibu wa Mamlaka aliyopewa chini ya kifungu Nam. 11 (2) (d) na kifungu cha 11 (3) cha Sheria ya Wakala wa Maendeleo ya Viwanda Vidogo Vidogo na vya Kati Zanzibar Namba 2 ya mwaka 2018 na umeanza tarehe 20 mwezi huu.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.