Habari za Punde

Maadhimisho ya siku ya watu Duniani


Na Khadija Khamis Maelez
Imeelezwa kuwa Zanzibar bado iko chini katika matumizi ya uzazi wa mpango ambapo ni asilimia 14 tu ya walengwa kati ya 32 wanajitokeza kupatiwa huduma hiyo kwa mwaka 2015-2016.
Akifungua Semina ya Waandishi wa Habari katika kuadhimisha siku ya Idadi ya Watu Duniani katika Ukumbi wa Sanaa Rahaleo Kamishna wa Tume ya Mipango Zanzibar Salama Ramadhani amesema lengo lililopangwa ni kufikia asilimia 20 ifikapo mwaka 2020 lakini inaonekana idadi bado iko chini ikilinganishwa na kanda ya kusini ya Tanzania bara kumefikia matumizi ya aslimia 51 na kwa upande wa nyanda za juu kusini imefikia asilimia 44.
Amesema hali inaonyesha kuwa katika Mikoa ya Zanzibar,Mkoa wa Kusini Pemba unamatumizi madogo zaidi katika njia za kisasa za uzazi wa Mpango ambapo hadi sasa ni asilimia 6.8 ya watu wanaotumia njia hizo.
Ameutaja Mkoa wa Kusini Unguja unaongoza kwa kuwa na asilimia  28.9 ya watumiaji wa njia hizo za uzazi wa mpango na kupelekea kuleta faraja kwa jamii na Taifa kwa ujumla.
Alieleza uzazi wa mpango ni haki ya kila mtu husaidia kupunguza vifo kwa akinamama wajawazito na kuimarisha afya ya mama na mtoto vilevile huisaidia serikali kuimarisha huduma za jamii kama  elimu miundombinu na huduma za afya.
Kamishna huyo alisema wanaume wameonekana kuwa ni kikwazo kikubwa katika kufikia malengo ya uzazi wa mpango kutokana na mwamko mdogo wa elimu na kuwaomba wataalamu na wanaharakati kutoa nguvu za ziaza kwa kuwaelimisha juu ya njia hizo.
 “Wanaume wamekuwa ni kiwazo katika kufikia malengo kwani wamekuwa wagumu kuwaruhusu wake zao kujiunga na hata wengine kutishia kutoa Talaka”,Alisema Kamishna Salama.
Hata hivyo  Alisema iwapo elimu ya uzazi wa mpango itawafikia zaidi wanaume wakaelewa azma ya taifa juu ya uzazi wa mpango basi mkakat wa kupunguza vifo vya kina mama na watoto wachanga unaweza kufanikiwa kw kiasi kikubwa .
Nae Mratibu wa Huduma za Afya ya Uzazi  na Mtoto kutoka Wizara ya Afya Dkt. Wanu Bakar Khamis alisema uzazi wa mpango na maendeleo ni haki ya kila binaadamu hivyo ni muhimu kupanga uzazi ili kuweza kabaki na familia ndogo ambayo itapata huduma nzuri, na malezi bora kwa watoto na kupelekea wanafamilia kufurahia maishaya ndoa yao.
Alisema akina mama wamekuwa wakiapoteza nguvu nyingi wakati wa ujauzito na kujifungua hivyo iwapo watajiunga na njia za uzazi wa mpango wataweza kuzirudisha kwa kupata kupata muda nzuri wa kunyonyesha watoto na kuwa na furaha na kuwapatia lishe bora.
Nae Mkufunzi kutoka chuo kikuuu cha Taifa Zanzibar (SUZA) Dkt. Issa Haji Ziddi amesema uzazi wa mpango unakubalika katika dini ili familia ziweze kujenga maisha bora kiuchumi ,kisiasa,utamaduni na kiafya sambamba na kuwaptuia watoto malezi bora.
Siku ya watu duniani huadhimishwa kila mwaka ifikapo tarehe  11  mwezi wa saba duniani kote na kwa upande wa Zanzibar inatarajiwa kufanyika katika Ukumbi wa Sheikh Idrisa Abdul-wakiil Kikwajuni na Mgeni Rasmi anatarajiwa kuwa Makamo wa Pili wa Rais Balozi Seif Ali Idd ambapo kauli mbiu ya mwaka huu ni  “Uzazi wa mpango ni haki ya binadamu .”
   Imetolewa na Idara ya Habari maelezo Zanzibar.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.