Habari za Punde

Michezaji wa Zamani wa Timu ya Jamuhuri ya Kisiwani Pemba Afariki na Kuzikwa Jana Kijijni Kwao.

Na. Abdi Suleiman, PEMBA
TIMU ya Jamhuri, imesema imepokea kwa masikitiko makubwa, kifo cha aliyekuwa mchezaji watimu hiyo, Ahmed Salum Said, aliyefariki dunia kwa ajali ya Vespa mjini Unguja.
Marehemu Ahmed aliwahi kuitumiakia timu hiyo katika miaka ya 1988-1995, wakati alipokuwa akicheza beki nne katika timu hiyo na kufanya vyema wakati huo.
Akizungumza na pembatoday, Meneja wa Timu hiyo yenye maskani yake Chasasa Wete, Abdalla Mohamed Elisha alisema, uongozi wa Jamhuri umepokea kwa masikitiko, kwani alikuwa tegemeo kwa timu yao.
Alisema katika uhai wake marehemu alikuwa akiendelea kuiunga mkono timu yao, kwa hali namali hata ushauri na suala zima la usajili wa wachezaji wapya.
“Pengo kubwa kwetu ila Mwenyezi Mungu ndio amepanga litokee, sisi tutaendelea kumkumbuka daima kutokana na michego yake na msimamo wake katika timu,”alisema.
Elisha alifahamisha kuwa, marehemu wakati wa uhai wake aliwahi kucheza pamoja na wazaji nguli, katika miaka hiyo, akiwemo Abdalla Mtwango, Omar Mkubwa Too, Abdalla Karimu na hata marehemu William John.
“Sisi tumepata taarifa jana jioni kuwa, marehemu amepata ajali ya vespa na amefariki dunia, marehemu amezikwa katika makaburi ya kijijini kwao Kinuni Unguja, Viongozi wa Jamhuri tumeshiri,ki kwa kiasi kukubwa katika mazishi ya Mchezaji huyo”alisema.
Hata hivyo Elisha alisema kuwa uongozi wa Jamhuri uko bega kwa bega na familia ya marehemu, Ahmed Salum Said, katika kipindi hiki kigumu kwao.
  Allah, ailaze roho ya marehemu pahala pema peponi amini…..

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.