Habari za Punde

Ujumbe Maalum wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Ukishiriki Sherehe Rasmin ya Uwekaji Mkuku wa Meli Mpya ya Mafuta.

"Leo siku ya tarehe 9 Julai 2018, Ujumbe Maalum wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar ulishirika katika Sherehe rasmi ya uwekaji wa mkuku ( _Keel Laying Ceremony)_ wa meli mpya ya mafuta huko katika _Shipyard_ ya Kampuni ya DAMEN ya Uholanzi ambayo ipo katika Mji wa *Yichang* kwenye Jimbo la *Hubei* nchini **China* . Ujenzi wa Meli hiyo ambao umeanza kwa kukatwa vyuma na kuviunganisha na kuwekwa mkuku unategemea kumaliza katika mwezi wa *June 2019*".

"Meli hiyo mpya itakuwa na uwezo wa kuchukuwa tani *3,500* za mafuta ya aina ya __Diesel, Petrol, Kerosene na Jet A1_ na inategemewa kuja kuongeza nguvu kwa kusambaza mafuta katika bandari za Mwambao wa East Afrika kuchukuwa nafasi ya MT Ukombozi iliyojengwa na Serikali 1980 hujo Japan.

Ujumbe huo wa Serikali uliongozwa na Mh Khalid Moh'd (Waziri wa Fedha na Mipango) akifuatana na Dk Sira Ubwa Mamboya (Waziri wa Ujenzi, Mawasiliano na Usafirishaji pamoja na Mh Said Hassan (Mwanasheria Mkuu wa Zanzibar). Wengine walioshiriki ni Nd. Juma Reli (Katibu Mtendaji wa Tume ya Mipango), Nd. Khamis Mussa (Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango) na Nd. Mustafa Jumbe (Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Mawasiliano na Usafirishaji) pamoja na Nd. Salum Ahmada (Mkurugenzi Mwendeshaji wa Shirika la Meli Zanzibar)

Aidha wengine waliohudhuria ni Mh. Mbelwa Kairuki (Balozi wa Tanzania nchini China akifuata na Nd. Lusekelo S. Gwassa kutoka Ofisi ya Ubalozi wa Tanzania nchini China







No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.