Katibu Mkuu Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar Mhe. Dkt. Idrissa Muslim Hija, akizungumza na kutowa nasaha zake kwa Wanafunzi Waliofanya vizuri Mitihani yao ya Kidatu cha Sita kwa mwaka 2017/2018 kwa kupata Daraja la Kwanza, wakati wa hafla ya kukabidhiwa zawadi na Uongozi wa PBZ kwa kufanya vizuri mitihani yao na kujiandaa na Elimu ya Juu.
KATIBU Mkuu wa Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali
Zanzibar Idrissa
Muslim Hija amewataka wahitimu wa kidatu cha sita wasome kwa
mashirikiano,waondokana na ubinafsi na wahakikishe wanakuwa na marafiki wema ili kupata mafanikio waliyoyakusudia.
Aliyasema hayo katika sherehe ya
kukabidhiwa zawadi za fedha na Benki ya Watu wa Zanzibar Ltd kwa
wanafunzi wa kidatu cha sita waliofaulu daraja la kwanza kwa Skuli za Sekondari
za Unguja na Pemba,katika viwanja vya Kariakoo mjini hapa.
Alisema masomo ya ngazi ya juu
daraja la kwanza ni magumu hivyo inahitajika juhudi na mikakati iliobora ili
waweze kufaulu vyema.
Aliwataka wanafunzi hao kujenga ari,hamasa na bidii zaidi katika
masomo yao ili kuijengea heshima nchi yao ya Zanzibar hasa ikizingatiwa dharau
si jambo jema.
“Ubinafsi epukeni nao kwani siku zote hauleti neema nawaombeni
mnapokwenda shirikianeni,saidianeni muweze kufanikiwa “,alisisitiza.
Aidha aliwashauri wanapomaliza masomo wahakikishe wanarejea nyumbani
kwao kwani taifa linawahitaji kwa ajili ya uimarishaji wa maendeleo na
uchumi.
No comments:
Post a Comment