Habari za Punde

Msanii wa Kikundi cha Sanaa cha JKU Zanzibar Afariki Dunia na Kuzikwa Kijijini Kwao Wilayani Kondoa Dodoma.

MSANII  wa maigizo ya filamu  zanzibar katika kundi la jku art group  HAWA  RAMADHAN SARIA  amefariki dunia katika hospitali ya mnazi mmoja   baada ya kuugua kwa muda mfupi .

Kwa mujibu wa maelezo kutoka kwa msimamizi   mwongozaji  wa   kikundi cha maigizo  jku art group haji kimtende  amesema  marehemu  hawa  alianza kujisikia vibaya kiafya  na hatimae kupelekwa hospitali ya mnazi mmoja kwa ajili ya matibabu zaidi  lakini hali yake haikuwa nzuri hadi  mauti yalipomkuta siku ya  jumatano 22/8/2018.

Mwili wa  marehemu umesafirishwa leo alhamis  23/8/2018  na kupelekwa nyumbani kwao    MKOANI DODOMA WILAYA KONDOA  kwa shughuli za  mazishi

Marehemu    amejiunga na kikundi cha  sanaa  ya maigizo  cha  jku  mwanzoni  mwa mwaka 2015 , na  ameshiriki katika  tamthilia  mbili  na filamu  moja  za kikundi hicho ikiwemo  mchezo ulijipatia umaarufu  mkubwa  kwa wapenzi wa tamthilia hapa  kama  mkombozi  na  tamthilia ya  kitendawili  ambayo  inaendelea kuoneshwa hewani kupitia  zbc  tv  pamoja na filamu  inayofahamika    chozi langu

Marehemu   hawa  ameacha mume , mwenyezimungu ailaze roho ya marehemu mahala pema peponi amiiiiiin.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.