Viongozi wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar wakiongozwa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe,Issa Haji Ussi (kushoto)wakiwa wamekutana na Ujumbe wa Wataalamu kutoka Nchi za Falme za Kiarabu Ukiongozwa na Waziri wa Nchi na Ushirikiano wa Kimataifa wa Muungano wa Falme za Kiarabu (UAE)Reem Ibrahim Alhashimy wakijadiliana mambo mbalimbali na sekta mbalimbali ambazo wanaweza kusaidia mkutano uliofanyika Hoteli ya Park Hyyat Shangani mjini Zanzibar.
Waziri wa Nchi na Ushirikiano wa Kimataifa wa Muungano wa Falme za Kiarabu (UAE)Reem Ibrahim Alhashimy wapili kushoto akizungumza katika mkutano uliowakutanisha Viongozi wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar wakiongozwa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe,Issa Haji Ussi na Ujumbe wa Wataalamu kutoka Nchi za Falme za Kiarabu kuhusiana na mambo mabalimbali na sekta mbalimbali ambazo wanaweza kusaidia mkutano uliofanyika Hoteli ya Park Hyyat Shangani mjini Zanzibar.
Waziri wa Nchi na Ushirikiano wa Kimataifa wa Muungano wa Falme za Kiarabu (UAE)Reem Ibrahim Alhashimy akizungumza na Waandishi wa Habari baada ya kumaliza Mkutano uliowakutanisha Viongozi wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar wakiongozwa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe,Issa Haji Ussi na Ujumbe wa Wataalamu kutoka Nchi za Falme za Kiarabu kuhusiana na mambo mabalimbali na sekta mbalimbali ambazo wanaweza kusaidia mkutano uliofanyika Hoteli ya Park Hyyat Shangani mjini Zanzibar.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe,Issa Haji Ussi akizungumza na Waandishi wa Habari baada ya kumaliza Mkutano uliowakutanisha Viongozi wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar na Ujumbe wa Wataalamu kutoka Nchi za Falme za Kiarabu kuhusiana na mambo mabalimbali na sekta mbalimbali ambazo wanaweza kusaidia mkutano uliofanyika Hoteli ya Park Hyyat Shangani mjini Zanzibar.
Kiongozi wa Wajumbe kutoka Falme za kiarabu (UAE)Mshauri wa Waziri wa Nchi Ushirikiano wa Kimataifa Serikali ya Falme za Kiarabu Najla Alkaabi akizungumza katika mkutano maalum wa watendaji wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kuhusiana na maswala mbalimbali ya miradi ya Serikali katika ukumbi wa Ofisi ya Mtakwimu Mkuu wa Serikali mazizini Magharibi B Unguja.
Katibu Mkuu Wizara ya Biashara na Viwanda Juma Ali Juma akizungumza na Waandishi wa Habari mara baada ya kumalizika kwa mkutano maalum wa watendaji wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar na Ujumbe wa Wataalamu kutoka Falme za kiarabu (UAE)kuhusiana na maswala mbalimbali ya miradi ya Serikali katika ukumbi wa Ofisi ya Mtakwimu Mkuu wa Serikali mazizini Magharibi B Unguja.
Picha na Yussuf Simai /Maelezo Zanzibar.
No comments:
Post a Comment