Habari za Punde

EPL: Liverpool Yailaza Tottenham, Arsenal, Chelsea na ManCity Zawika

Mkufunzi wa Liverpool Jurgen Klopp amesema kuwa kikosi chake kilihitaji ushindi huo mkubwa baada ya kuilaza Tottenham na kujipatia ushindi wa tano katika awamu ya kwanza ya msimu tangu 1990.
Liverpool ilionyesha kiwango cha mchezo mzuri kufikia sasa katika uwanja wa Wembley katika ushindi uliowaweka wakiwa na pointi sawa na Chelsea ambao wako juu ya jedwali la ligi kupitia tofauti ya mabao.
Georginio Wijnaldum alifunga bao lake la kwanza la ugenini tangu alipojiunga na Liverpool - huku teknolojia ikidai kwamba bao la kichwa alilofunga lilikuwa limepita mstari wa goli licha ya jaribio la kipa wa Spurs Michel Vorm kulipangua.
Wageni hao walitawala mchezo katika kila nyanja na kuongeza uongozi wao baada ya dakika 54, wakati Roberto Firmino alipofunga kutoka katika mstari baada ya beki Jan Vertongen kuchanganywa na mpira wa krosi uliopigwa na Mane katika goli lake.
Wakati huohuo mpira wa adhabu uliopigwa na Granit Xhaka uliiweka Arsenal kifua mbele katika ushindi wa tatu chini ya mkufunzi Unai Emery huku Newcastle ikisalia bila ushindi wowote wa ligi ya Premia.
Licha ya kusumbuliwa katika kipindi cha kwanza , Xhaka aliiweka kifua mbele The Gunners kupitia mpira wa adhabu ambao ulimpita kipa wa Newcastle Martin Dubravka.
Huku wageni wakizidisha matumaini, Mesut Ozil alifunga bao la pili na kuihakikisha Arsenal inashindi mechoi mbili za ugenini mfululizo kwa mara ya kwanza tangu 2017.
Eden hazard alifunga mabao matatu huku Chelsea ikiicharaza Cardiff City ili kuendeleza matokeo ya asilimia 100 tangu kuanza kwa ligi ya Uingereza hatua iliowafanya kupanda juu ya jedwali.
Wageni hao waliopandishwa daraja walipata bao la uongozi wakati mpira wa adhabu wa Joe Ralls ulipopigwa kichwa na nahodha wao Sean Morrison hadi kwa Sol Bamba ambaye alicheka na wavu.
Hatahivyo, Hazard alifunga mara mbili katika kipindi cha dakika saba kabla ya kipindi cha kwanza na kuipeleka Chelsea katika kilele cha jedwali la ligi.
Leroy Sane aliadhimisha kurudi kwake katika kikosi cha kwanza cha Man City baada ya mabingwa hao watetezi kuilaza Fulham na kuimarisha matokeo mazuri bila kushindwa katika ligi ya Uingereza.
Sane, ambaye alikuwa akianza mechi yake ya kwanza ya ligi alifungua orodha ya mabao katika dakika mbili baada ya kufunga kufuatia pasi ya Fernandinho.
David Silva alifunga bao la pili kabla ya kipindi cha kwanza kukamilika, huku naye Raheem Sterling akiihakikishia timu yake ushindi huo dakika mbili kabla ya kipindi cha kwanza kukamilika.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.