Habari za Punde

Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Magufuli Aendelea na Ziara Yake Mkoani Mara. Aweka Jiwe la Msingi Mradi wa Ujenzi wa Barabara ya Makutano ya Nyamuswa - Sanate - Nata - Ikoma Gate KM 135, ehemu ya Makutano - Sanzate 50 KM. Butiama Mkoani Mara.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akivuta utepe pamoja na Mama Maria Nyerere mke wa Hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere ili kuweka jiwe la msingi mradi wa ujenzi wa Barabara ya Makutano-Nyamuswa- Sanzate-Nata-Ikoma gate km 135 katika sehemu ya Makutano-Sanzate km 50 katika sherehe zilizofanyika Butiama mkoani Mara. 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akimshukuru Mama Maria Nyerere mke wa Hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere mara bada ya kuweka jiwe la msingi mradi wa ujenzi wa Barabara ya Makutano-Nyamuswa- Sanzate-Nata-Ikoma gate km 135 katika sehemu ya Makutano-Sanzate km 50 katika sherehe zilizofanyika Butiama mkoani Mara.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na wananchi wa Butiama(hawaonekani pichani) kabla ya kuweka jiwe la msingi mradi wa ujenzi wa Barabara ya Makutano-Nyamuswa- Sanzate-Nata-Ikoma gate km 135 katika sehemu ya Makutano-Sanzate km 50 katika sherehe zilizofanyika Butiama mkoani Mara.
 Kikundi cha ngoma za asili cha Engubha cha kabila la wakabwa wenyeji wa Butiama mkoani Mara kikitumbuzia katika sherehe hizo 

Mzee Joseph Butiku akiwa amekaa na Mwanasiasa mklongwe Stephen Wassira pamoja na viogozi wengine wakifatilia kwa makini hotuba ya Rais Dkt. Magufuli katika sherehe hizo za uwekaji wa jiwe la msingi Butiama mkoani Mara. Picha na Ikulu.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.