Habari za Punde

SMZ hukutana na maafisa wa Kazi wa mikoa kutathmini utendaji wa Kamisheni

Na Takdir Ali na Kijakazi Abdalla-Maelezo Zanzibar 
Waziri wa Kazi,Uwezeshaji Wazee,Wanawake na Watoto Moudline Castico amesema Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar hukutana mara kwa mara na Maafisa wa kazi wa Mikoa ili kutathmini utendaji wa Kamisheni ya kazi hasa kwa Taasisi binafsi.
Lengo na Mikutano hiyo ni kutafuta njia za kuepusha migogoro inayojitokeza miongoni mwa Wafanyakazi na Waajiri.
Waziri Castico ameyasema hayo alipokuwa akisoma Ripoti ya Utekelezaji wa maoni ya Kamati ya Maendeleo ya Wanawake,Habari na Utalii ya Baraza la Wawakilishi mwaka 2017-20118,huko katika Ukumbi wa Baraza la Wawakilishi Chukwani.
Amesema Serikali kupitia Wizara imekuwa ikipokea malalamiko ya mara kwa mara inayohusiana na wafanyakazi hivyo Wizara imeandaa mikakati maalumu ya kupambana na suala hilo.
Waziri Castico amesema Wizara imekuwa kipokea tuhuma na malalamiko mbalimbali na kuzifanyia kazi kwa mujibu wa Taratibu na Sheria zilizowekwa.
Hata hivyo amesema mwaka 2018-2019,Kamisheni ya Kazi imepanga kukagua kiasi ya wastani wa Taasisi 600 ikilinganishwa na Wastani wa 297 mwaka 2017/2018.
Aidha amesema Wizara kupitia kamisheni ya kazi imenunua gari kwa ajili ya kuongeza kiwango cha ukaguzi ili kuimarisha ufanisi wa kazi hizo.
Mbali na hayo Mheshimiwa Castico amesema Serikali imetengeneza Sera ya ajira ya mwaka 2009 na miongozo na Sheria ya Mamlaka ya Uwekezaji Vitega Uchumi Zanzibar (ZIPA) nambari 11 ya mwaka 2004 inayotoa maelekezo ya kupewa kuipa umbele kwa wazalendo katika masula ya ajira.
Akitoa maoni ya Kamati ya Maendeleo ya Wanawake,Habari na Utalii ya Baraza la Wawakilishi Mwenyekiti wa Kamati hiyo Mwantatu Mbaraka Khamis amesisitiza kwa waajiriwa wa kamisheni ya kazi kufuata Sheria,Kanuni na maadili na miongozo ya kazi ili kupunguza migogoro katika sehemu za kazi.
Akielezea kuhusu makato ya wafanyakazi katika Mfuko wa Hifadhi ya Jamii Zanzibar (ZSSF) Mwantatu ameitaka Wizara hiyo kufutilia ili kuhakikisha makato hayo yanafikishwa katika sehemu husika.
Wakichangia ripoti hiyo Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar wameiomba Serikali kutoa Kipa umbele kwa wazawa wakati wanapotoa ajira kwa wale wenye sifa na uwezo ili kuhakikisha wanafaidika na matunda ya nchi yao.
Imetolewa na Idara ya Habari Maelezo Zanzibar.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.