Habari za Punde

Maadhimisho ya Sherehe za Skuli ya Sekondari na Msingi Trifonia Academy Founi Zanzibar Kutimia Miaka 20 na Mahafali ya 13 ya Skuli Hiyo.

Waziri wa Kazi Uwezeshaji Wazee Wanawake na Watoto Zanzibar Mhe., Maudline Castiko akiongozana na Mkurugenzi wa Skuli ya Trifonia Bi Grace Peter wakielekea katika eneo la sherehe hiyo wakati akiwasili katika viwanja hivyo kuhudhuria Maadhimisho ya Sherehe za Miaka 20 ya Skuli hiyo na Mahafali ya 13 ya Kidatu cha Nne na Darasa la Sita.
Waziri wa Kazi Uwezeshaji Wazee Wanawake na Watoto Zanzibar Mhe. Maudline Castico akisalimiana na Wanafunzi wa Maandalizi wa Skuli hiyo baada ya kuonesha michezo yao wakati wa hafla ya Maadhimisho ya kusherehekea Miaka 20 na Mahafali ya 13 ya Skuli hiyo yaliofanyika katika Viwanja vya Skuli hiyo huko Fuoni Zanzibar.
Waziri wa Kazi Uwezeshaji Wazee Wanawake na Watoto Zanzibar Mhe. Maudline Castico akiwahutubia Wazazi na Wahitimu wa Kidatu cha Nne na wa Darasa la Sita baada ya kumaliza masomo yao wakati wa hafla ya Mahafali ya 13 ya Skuli hiyo ya Trifonia Academy Fuoni Zanzibar, akimuwakilisha Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar Mhe. Riziki Juma Pemba, hafla hiyo imefanyika katika viwanja vya Skuli hiyo Fuoni Wilaya ya Magharibi B Unguja. 

Wazazi wa Wanafunzi na Wageni waalikwa wakifuatilia hafla hiyo ya Madhimisho ya Miaka 20 ya Skuli hiyo na Mahafali ya 13 ya Wanafunzi wa Kidatu cha Nne na Darasa la Sita.wakimsikiliza Mgeni rasmin akitowa nasaha zake kwa Wahitimu hao.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.