Habari za Punde

Corinne Hutton: Mwanamke mlemavu aweka historia Mlima Kilimanjaro

Corinne Hutton (kulia) alisindikizwa na watu 10 kutoka shirika la Finding Your Feet

Mwanamke ambaye hana miguu na wala hana mikono ya kuzaliwa nayo anaaminika kuwa mtu wa kwanza wa aina hiyo hufika katika kilele cha Mlima Kilimanjaro.
Corinne Hutton, 48, kutoka eneo la Renfrewshire, alipoteza mikono na miguu yake baada ya kuugua sana ugonjwa wa kichomi na ugonjwa wa septicaemia ambao huhusisha mtu kuwa na sumu katika damu mwaka 2013. Madaktari wakati huo walisema uwezekano wake kunusurika ulikuwa asilimia tano.
Alitumia siku tano kufika kileleni.
Alifika katika kilele cha mlima huo mrefu zaidi barani Afrika Ijumaa, akiwa ameandamana na watu 10 kutoka kwenye shirika la kuwasaidia watu walipoteza miguu na mikono la Finding Your Feet.
Walifanikiwa kuchangisha zaidi ya £30,000 za kusaidia shirika hilo la hisani alilolianzisha baada yake kuugua.
Kundi hilo lilimaliza kushuka kutoka kwenye mlima huo ulio na urefu wa 16,100ft (4,900m) Jumapili asubuhi.
Bi Hutton alisema alikuwa na malengelenge kwenye miguu yake kuanzia siku ya kwanza.
"Kila asubuhi, ilinilazimu kuvalia miguu yangu bandia na kufanya hivyo tena na tena.
"Nimekuwa wakati mwingine naishiwa na pumzi, hata nikiwa sipandi mlima. Nilikuwa na kikozi kikali ambacho kimekuwa kiliendelea kuwa kibaya siku baada ya siku, lakini nilikuwa tu nauweka mguu mmoja mbele ya ule mwingine na kusonga. Na nilijua kwamba hakuna jambo lingenizuia kufika kileleni.
"Natumai kwamba nitawatia moyo watu wengine kujitokeza na kuikwea milima yao, milima ya aina yote.
"Nilisema baada ya kukatwa miguu yangu chini ya magoti na mikono pia kwamba sikutaka kamwe kuchukuliwa kama 'mlemavu' na nafikiri kwamba nimethibitisha hilo wikendi hii."
Bi Hutton anasema alikuwa na malengelenge miguuni tangu siku ya kwanza.
Anasema anataka kuwahamasisha watu wengine kuwaambia kuwa wanaweza "kuipanda milima yao"
Kupitia taarifa katika ukurasa wao wa Facebook, shirika la Finding Your Feet (Kuipata Miguu Yako) limesema "kila mmoja wao yuko nasi hapa kwenye kilele hiki".
Waliongeza: "Tulikwenda kulala tukiwa hatuna chochote kutoka mlimani ila wasiwasi.
"Walikabiliana na ukosefu wa hewa ya kutosha, giza na baridi kali."Tunaamini Corinne ndiye mwanamke wakwanza aliyekatwa miguu na mikono kufika kileleni Kilimanjaro... ni ufanisi mkubwa sana bila miguu na mikono."

Bi Hutton, anayeishi Lochwinnoch, awali alikuwa ameweka historia yakuwa mwanamke wa kwanza asiye na miguu na mikono kupanda mlima Ben Nevis.
Mwaka 2017, alitolewa sehemu kubwa ya pafu lake moja baada ya kuambukizwa.
Alijiandaa kukwea Mlima Kilimanjaro ndani ya chumba maalum kinachoiga mazingira magumu ya mlimani katika Chuo Kikuu cha Scotland Magharibi.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.