Habari za Punde

Jumuiya ya Pemba Foundation na Mwakilishi wa Jimbo la Micheweni Pemba Wachangea Sekta ya Elimu Kisiwani Humo.

Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar Mh. Rizki Pembe Juma akiishukuru Jumuiya ya Pemba Foundation pamoja na Mwakilishi wa Jimbo la Micheweni Mh. Shamata kwa juhudi zao za kuunga mkono Sekta ya Elimu.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe. Balozi Seif akizungumza na Wanafunzi wa Skuli ya Maziwang’ombe mara baada ya kuweka Jiwe la Msingi la Skuli ya Maandalizi ya Maziwang’ombe.Kisiwani Pemba wakati wa ziara yake ya Kikazi Pemba.
Baadhi ya Wanafunzi wa Skuli ya Maandalizi ya Maziwang’ombe wakimsikiliza Balozi Seif akiwanasihi kupenda kujishughulisha na masomo yao na kuacha mchezo.
 Weanafunzi wa skuli ya Msingi ya Micheweni wakitulia kumsikiliza Balozi Seif huku wakiwa na shauku ya kusubiri kukabidhiwa zawadi zao za Mikoba, mashungi, Penseli pamoja na Kampasi zilizotolewa na Mfanyabiashara Said Naaser Boopar.
 Wanafunzi wa skuli ya msingi ya Micheweni wakitoa burdani ya wimbo maalum wa kuwapongewa Viongozi na Wafadhili waliojitolea kusaidia maendeleo ya skuli yao ikiwemo vifaa na zawadi mbali mbali.
 Balozi Seif akiwa na Waziri wa Elimu akijaribu moja miongoni mwa viti sita vilivyowekwa ndani ya Darasa la Chuo cha Kiislamu Micheweni alipofika kukagua ujenzi wa Madarasa sita ya Chuo hicho.
Balozi Seif akimkabidhi Daktari dhamana wa Hospitali ya Micheweni Dr. Mbwana Shoka vifaa mbali mbali vya Hospitali vilivyotolewa na Mfanyabishara Mzalendo Said Naaser Boopar.

Picha na – OMPR – ZNZ.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.