Habari za Punde

Mkutano wa Vijana wa UVCCM Kumpigia Kampeni Mgombea Uwakilishi wa CCM Jimbo la Jangombe.Ndg. Ramadhan Hamza Chande.

Vijana wa Chama Cha Mapinduzi Jimbo la Jangombe wakishangilia wakati wa Mkutano wa Kampeni ya Uwakilishi Jimbo la Jangombe wakishangilia wakati wa Mkutano wa Kampeni ya Mgombea Uwakilishi kupitia CCM Ndg. Ramadhan Hamza Chande katika viwanja vya Tawi la CCM Kigongochekundu Zanzibar.
Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi kupitia Nafasi za Vijana wakisalimia na kumpigia debe na kumuombea Kura Mgombea wa Uwakilishi Jimbo la Jangombe wakati wa Mkutano wa Kampeni ulioandaliwa na UVCCM katika viwanja vya Tawi la CCM Kidongochekundu Zanzibar.
Vijana wa CCM wakifuatilia Mkutano wa Kampeni ya Uchaguzi Mdogo wa Jimbo la Jangombe Zanzibar uliofanyika katika viwanja vya Tawi la CCM Kidogochekundu Zanzibar. 
Mjumbe wa UVCCM Ndg. Abdulhafar, akihutubia na kumuombea Kura Mgombea wa CCM katika Uchaguzi Mdogo wa Jimbo la Jangombe Ndg. Ramadhan Hamza Chande. katika viwanja vya Tawi la CCM Kidongochekundu Zanzibar. 
Mwakilishi wa Jimbo la Welezo Zanzibar Mhe Hassan Diaspora akihutubia na kumuombea Kura Mgombea wa CCM katika Jimbo la Jangombe Zanzibar Ndg. Ramadhan Hamza Chande akisisitiza jambo wakati wa mkutano wa Kampeni katika viwanja vya Tawi la CCM Kidongochekundu. 
Mmoja wa Waliowania nafasi ya kuchanguliwa kupeperusha Bendera ya CCM katika kinyanganyiro cha kuwania kuchaguliwa kugombea nafasi ya Uwakilishi katika jimbo hilo ngazi ya Jimbo Othman Kibwani, akimuombea Kura Ngombea wa CCM katika uchaguzi mdogo wa Jimbo la Jangombe Ndg. Ramadhan Hamza Chande.katika viwanja vya Tawi la CCM Kidongochekundu Zanzibar. 
Mwanachama wa CCM ambaye alijitokeza kuwania nafasi hiyo kuchaguliwa kugombea kupitia CCM Ndg. Taifan Vuai Makame, akimkabidhi CD ya Kumbukumbu za Mapinduzi ya Zanzibar Katibu Mkuu wa UVCCM Ndg. Raimond Mangwala, wakati wa mkutano wa Kampeni ya kumnadi mgombea wa CCM Jimbo la Jangombe.  No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.