Habari za Punde

Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Mjini Magharibi atoa taarifa kwa waandishi juu ya azimio la kikao cha kamati ya siasa

 Mwenyekiti wa Mkoa wa Magharib Kichama Mohamed Rajab Said wa kwanza (kushoto) akitoa taarifa kwa Waandishi wa habari juu ya Azimio la kikao cha kamati ya Siasa ya Mkoa wa Magharib huko Mwera katika Ukumbi wa CCM Mkoa wa Magharib.
 Mwenyekiti wa Mkoa wa Magharib Kichama Mohamed Rajab Said wa Pili (Kulia)akiskiliza Masuali kwa Waandishi wa habari (hawapo Pichani) yanayohusu taarifa ya Azimio la kikao cha kamati ya Siasa ya Mkoa wa Magharib huko Mwera katika Ukumbi wa CCM Mkoa wa Magharib.
Baadhi ya Waandishi wa habari wakiskiliza maelezo kwa Mwenyekiti wa Mkoa wa Magharib Kichama Mohamed Rajab Said (hayupo Pichani) alipokua akitoa taarifa kwa Waandishi wa habari juu ya Azimio la kikao cha kamati ya Siasa ya Mkoa wa Magharib .
Picha na Maryam Kidiko – Maelezo Zanzibar.

Na Mwashungi Tahir     Maelezo    12-10-2018.
Mwenyekiti  wa Mkoa wa Magharibi Kichama  Mohamed Rajab Said alisema jukumu la Chama Cha Mapinduzi kusimamia Serikali na kutizama kwa ukaribu kabisa mwenendo na maadili  ya Viongozi.
Alisema ili kutimiza kwa vitendo kauli ya Mwenyekiti wa chama cha Mapinduzi DR John Pombe Magufuli na Makamo Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi Dr Ali Mohamed Shein pia na Katibu Mkuu wa wa CCM Dr Bashiru na Dr Mabodi kwa Zanzibar ambao kila siku walikuwa wakiwaasa na kuhimiza viongozi wa chama wawe waadilifu .
Akizungumza  na waandishi wa Habari huko Mwera kwenye ukumbi wa CCM  Mkoa wa Magharibi A kwenye mkutano wa Azimio la kikao cha kamati ya siasa ya Mkoa kuhusu tuhuma alizozitoa Mwakilishi wa Baraza la Wawakilishi Mh Nadir.
Akitoa ufafanuzi juu ya mchango uliotolewa mbele ya Baraza la Wawakilishi na Mh Nadir kuhusu tuhuma nzito za uzushi zilizotolewa kwa mwenzetu wa kamati ya siasa Mkoa Magharibi kichama  ambapo sio kweli wala uthibitisho hakuna.
Hivyo Mwenyekiti alisema anaomba chama kichukuwe hatua zinazofaa baada ya kujiridhisha kwa tuhuma hizo na ikithibitika sheria ichukuwe kuanzia tawi hadi uongozi wa juu.
Alisema kiwanja hicho alipewa mjumbe huyo kisheria na vielelezo vyote vipo ikiwa kama ni fidia  ambapo kiwanja hicho kipo Mbweni kwani serikali haitoi ardhi kwa mwenye nguvu bali kinatoa kisheria.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.