Habari za Punde

Timu ya JKU Yaibuka Bingwa wa Kanda ya Unguja Mchezi wa Netiboli Kati Yake na Timu ya Mafunzo Kwa Kufungana Bao 39-38. Mchezo Uliofanyika Uwanja wa Gmykhana Zanzibar.

Mchezaji wa Timu ya JKU akiwa na mpira huku mchezaji wa Timu ya Mafunzo akijaribu kumzuiya wakati wa mchezo wao wa mwisho kutafuta Bingwa wa Ligi Kuu Kanda ya Unguja uliofanyika katika Uwanja wa Gmykhana Zanzibar.
Mchezo huo uliokuwa na upinzani wa hali ya juu kutokana na wachezaji wake kuwa makini katika ufungaji wa magoli kupitia kila upande wakipitana kwa bao moja kila mara hadi kota ya tatu timu ya JKU ikiwa mbele kwa mabao 29 - 28.
Kota ya nne ilipoaza Timu ya Mafunzo walikuwa wakiongoza Kota hiyo kwa mabao matatu mbele na Vijana ya JKU wakaweza kurudisha na kuibuka na ushindi wa mabao 39 -38 na Kutangazwa Mabingwa wa Mchezo wa Netiboli ligi Kuu Kanda ya Unguja na Timu ya Mafunzo kushika nafasi ya Pili ya Michuano hiyo.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.