Habari za Punde

Waziri wa Habari Utalii na Mambo ya Kale Zanzibar Azungumza na Waandishi wa Habari Kukamilika Kwa Tamasha la Kimataifa la Utalii Zanzibar (Tourisim Show) Litakalofanyika Katika Hoteli ya Verde Mtoni.

 
Waziri wa Habari, Utalii na Mambo ya Kale, Mhe.Mahmoud Thabit Kombo akizungumza na waandishi wa habari wa vyombo mbalimbali kuhusiana na maonesho ya utalii (Tourism show) yatakayofunguliwa  katika Hoteli ya Verde iliopo Mtoni Unguja , mkutano huo ulifanyika katika Hoteli ya Park Hyatt iliopo Shangani mjini Unguja
Katibu Mtendaji wa Kamisheni ya Utalii Zanzibar, Dk. Abdula Mohammed Juma akizungumza na waandhishi wa habari wa vyombo mbalimbali kuhusiana na ufunguzi wa maonesho ya utalii Zanzibar (Tourism show) yatakayofanyika katika Hoteli ya Verde MtoniMwandishi wa Habari wa Gazeti la Tanzania daima, Talib Ussi akiuliza suala katika mkutano  kuhusiana na ufunguzi wa maonesho ya utalii Zanzibar, uliofanyika katika Hoteli ya Park Hyatt iliopo Shangani
Tabia Makame mwandishi wa habari wa Redio ya Bahari Fm akiuliza suala katika mkutano  kuhusiana na ufunguzi wa maonesho ya Utalii Zanzibar, uliofanyika katika Hoteli ya Park Hyatt iliopo Shangani
Waziri wa Habari, Utalii na Mambo ya Kale Zanzibar Mhe. Mahmoud Thabit Kombo akifafanua jambo wakati wa mkutano na waandishi wa habari wa vyombo mbalimbali vilioko Zanzibar kuhusiana na kukamilika kwa maandalizi ya Tamasha la Kitalii Zanzibar linalotarajiwa kufanyika katika Hoteli ya Verde Mtoni Zanzibar,mkutano huo ulifanyika katika Hoteli ya Park Hyatt iliopo Shangani mjini Unguja
Mwenyekiti wa Bodi ya Kamisheni ya Utalii Zanzibar, Sabah  Saleh Ali akitoa ufafanuzi katika mkutano wa waandishi wa habari kuhusiana na ufunguzi wa maonesho ya Utalii Zanzibar (Tourism show), mkutano huo ulifanyika katika Hoteli ya Park Hyatt iliopo Shangani mjini Unguja
Meneja wa Hoteli ya Kitalii ya Park Hyatt,Mr.Nicolas Cedro akichangia katika mkutano wa waandishi wa habari ulijadili ufunguzi wa maonesho ya Utalii Zanzibar, yanayotarajiwa kufanyika tarehe 17/10/2018.
Waandishi wa habari wa Vyombo mbalimbali vya habari vilioko Zanzibar wakifuatilia Mkutano huo na Waziri wa Habari Utalii na Mambo ya Kale Zanzibar Mhe. Mahmoud Thaibt Kombo uliofanyika katika ukumbi wa Hoteli ya Kitalii ya Park Hyatt Shangani Zanzibar.
Waandishi wa Habari wa Vyombo mbalimbali vilioko Zanzibar wakifuatilia mkutano huo uliofanyika katika hoteli ya Park Hyatt Shangani Zanzibar.(Picha na Haroub Hussein)

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.