Habari za Punde

Benki ya Watu wa Zanzibar Limited Yakabidhi Msaada wa Mchele Kwa Ajili ya Kambi za Wanafunzi wa Kidatu cha Nne Kujiandaa ni Mitihani Yao ya Taifa Wilaya ya Kusini Unguja.

Afisa Muandamizi wa Masoko Benki ya Watu wa Zanzibar Limited Ndg. Mohammed Ismail Khamis,akimkabidhi msaada wa mchele kilo Elfu mbili (Tani 2) Mkuu wa Wilaya ya Kusini Unguja Mhe. Idrisa Kitwana Mustafa kwa ajili ya Kambi ya Wanafunzi wa Skuli za Wilaya ya Kusini Unguja wanaojiandaa kwa Mitihani yao ya Taifa ya Kidatu cha Nne, inayotarajiwa kuaza wiki ijayo Tanzania kote, makabidhiano hayo yamefanyika katika Ofisi ya Mkuu wa Wilaya Kusini Unguja Makunduchi.
Mkuu wa Wilaya Kusini Unguja Mhe Idrisa Kitwana Mustafa akitowa shukrani kwa Uongozi wa PBZ,kwa msaada wao huo kwa ajili ya matumizi ya chakula Wanafunzi wa Skuli za Wilaya ya Kusini wanaojiandaa na Mitihani yao ya Taifa ya Kidatu cha Nne wiki ijayo, hafla hiyo imefanyika katika viwanja vya Ofisi ya Mkuu wa Wilaya Makunduchi Wilaya ya Kusini Unguja.
Mkuu wa Wilaya ya Kusini Unguja Mhe. Idrisa Kitwana Mustafa akizungumza na waandishi wa habari kuhusiana na maandalizi ya Wanafunzi wa Wilaya yake katika kujiandaa na Mitihani yao ya Taifa ya Kidatu cha Nne, na kutowa maelezo Wanafunzi hao wamejiandaa na kuweza kufanya vizuri mitihani hiyo na kuibuka na division za kwanza kwa mwaka huu 2018.  
Afisa Muandamizi wa Masoko wa PBZ Ndg. Mohammed Ismail Khamis akizungumza na Mkuu wa Wilaya ya Kusini Unguja Mhe. Idrisa Ismail Khamis baada ya kumalizika kwa hafla ya kukabidhi msaada wa mchele tani mbili, katika viwanja vya Ofisi ya Mkuu wa Wilaya Makunduchi Zanzibar.
Imeandaliwa na Blog ya Zanzinews.com.
Othman Mapara.
0777424152. 

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.