Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Ali.Mohamed Shein, akizungumza na Rais wa Seychelles Mhe. Danny Faure, walipokutana kwa mazungumzo yaliofanyika katika ukumbi wa Hoteli ya Inter Continental Jijini Nairobi Nchini Kenya.
Na.Mwandishi Maaluum Nairobi.
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed
Shein, alikutana na kufanya mazungumzo na Rais wa Seychelles Danny Faure katika ukumbi wa
Hoteli ya Intercontinental Mjini Nairobi,na kueleza kwamba Zanzibar na Seychelles zina mazingira ya
kijiografia na shughuli za kiuchumi
zilizofanana na watu wa nchi hizo wamekuwa wakishirikiana katika shughuli mbali mbali za kiuchumi na kijamii.
Katika
mazungumo hayo, Dk Shein alihimiza haja ya kuimarisha uhusiano wa kidugu na
kihistoria uliopo baina ya nchi mbili hizo
Katika
kikao hicho Dk. Shein alikumbushia mambo
mbali mbali waliozungumza na Rais wa Zamani wa
Seychelles Mheshiwa James
Michel walipokutana wakati wa Mkutano
wa Nchi za Visiwa wa Samoa mwezi Septemba mwaka 2014.
Alisema viongozi hao walipokutana
walizungumza haja ya kuimarisha mashirikiano katika masuala mbali mbali ya
uchumi wa bahari, ikiwemo sekta ya utalii, uvuvi , usafiri wa anga na masuala,
kwa kuzingatia kwamba hayo ni maeneo muhimu ya kiuchumi kwa nchi
wanachama wa Jumuiya ya Nchi zinazopakana na Bahari ya
Hindi (IORA).
Dk.
Shein alisema kwamba itakuwa ni vyema Serikali iliyopo madarakani hivi sasa na
Rais Danny Faure ni vyema ikaendeza ushirikiano katika maeneo hayo na mengine mapya
kwa kuzingatia mahitaji ya wananchi na
mwenendo wa kiuchumi wa hivi sasa.
Aidha,
Dk Shein alileleza kwamba Serikali ya
Mapinduzi ya Zanzibar na Serikali ya
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania zitaendeleza kushirikiana na Serikali ya
Seychelles katika masuala ya ulinzi na
salama.
Vile
vile, alihimiza haja ya viongozi wa
pande hizo mbili kuwa na utaratibu wa
kutembeleana mara kwa mara,na kusisitiza haja ya viongozi pia kukutana pamoja kwa ajili ya kubainisha na
hatimae kutiliana saini maeneo ya ushirikiano
baina ya Seychelles na Zanzibar .
Kwa upande wake Mheshimiwa Danny Faure alitoa shukurani kwa Dk . Shein kwa kutenga muda maalumu wa
kukutana kwa ajili ya kujadili masuala muhimu ya kiuchumi na kijamii kwa ajili
ya kuimarisha ustawi wa wananchi wa pande mbili hizo.
Alieleza
kwamba ushirikiano biana ya Seychelles na Zanzibar una historia ndegu na
umezidi kuimairika baada ya kuundwa kwa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Alitoa
historia ya ushirikiano baina ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Seychelles
kabla ya nchi hiyo kupata uhuru mwaka 1976 na baada ya kupata huru.
Alieleza
kwama wananchi wa Seychelles wanakumbuka
na kuthamini mchango wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika masuala mbali
mbali ya kiuchumi, kiulinzi na kiusalama, na watahakisha wanaendeleza uhusiano
huo.
Alieleza
kwamba amefurahi kupata taarifa ya
mazungumzo aliyofanya Dk. Shein na Seychelles na Rais aliyeondoka
madaakani, James Michel
walipokutana wakati wa Mkutano wa Nchi
za Visiwa wa Samoa mwezi Septemba mwaka 2014.
Alisema kwamba maeneo ya ushiriakiano
waliyoyadili nchini Samoa ni muhimu na
Serikali yake iko tayari kuyaendeleza na kuongeza maeneo mapya ambayo yataonekana muhimu kwa
pande mbili hizo.
Alieleza
kwamba nchi yake iko tayari kushirikiana na Zanzibar katika kuimarisha sekta ya
utalii, biashara, uhifadhi wa mazingira, ulinzi na usalama na maeneo yote
muhimu katika kuendeleza uchumi endelevu wa bahari kama kwa kuzingatia malengo ya mkutano wa uchumi endelevu wa bahari uliowakutanisha viongoi hao
mjini Nairobi
Mheshimiwa Danny Faure nae alisititiza juu ya haja ya viongozi wakuu wa sekta mbali mbali wa Zanzibar na
Seychelles kukutana kwa ajili ya kujadili na hatimae kusaini
makubalino ya maeneo ya ushirikiano kwa faida ya pande zote mbili.
Viongozi hao waliagana kwa kila mmoja kumtakia mwenzake safari njema ya kurudi nyumbani.
No comments:
Post a Comment