Habari za Punde

SMZ Kushughulikia Masuala ya Utumishi wa Umma na Kutekeleza Mipango ya Kuleta Mabadiliko.

Na Raya Hamad OR-KSUUUB
Imeelezwa kuwa hatua mbalimbali za msingi zimechukuliwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar katika kushughulikia masuala ya Utumishi wa Umma na pia  imekuwa ikitekeleza mipango ya kuleta mabadiliko yaliyokusudiwa pamoja na mafaniko katika maeneo ya uchumi,usimamizi wa fedha ,kuimarisha taasisi za umma na rasilimali watu, huduma za kujamii na miundo mbinu.

Naibu Katibu Ofisi ya Rais Katiba Sheria Utumishi wa Umma na Utawala Bora Ndugu Seif Shaaban Mwinyi anaeshughulikia masuala ya utumishi ameeleza hayo wakati wa ufunguzi wa kikao cha kujadili mwelekeo wa mpango wa kuimarisha Utumishi wa Umma Zanzibar.

Ndugu Seif amesema  hatua za mpango wa kuimarisha Utumishi wa Umma ni muhimu kwa vile  Zanzibar imepata fursa ya kuingia awamu mpya ya utekelezaji,hivyo majadiliano hayo yatajielekeza katika hali halisi ilivyo sasa, changamoto na hatimae kupokea maoni na michango itayosaidia kuzingatiwa katika uandaaji wa program ya pili ya mabadilikoya utumishi wa umma Zanzibar.
 
Ndugu Seif ameeleza Mkakati wa Kukuza Uchumi na Kupunguza Umasikini  Zanzibar umeweka msisitizo wa kupatikana kiwango cha juu cha utawala bora na kuondokana na  umasikini pamoja na kutambua umuhimu wa nafasi ya usimamizi wa Utumishi wa Umma katika kuyafikia malengo ya maendeleo ya Zanzibar.

Pia alikumbushia na kusema kuwa uzinduzi wa Dira ya Maendeleo ya Zanzibar 2020 na MKUZA mwanzoni mwa mwaka 2000 zilileta hamasa na ari ya kutafuta mabadiliko ya kimaendeleo ikiwemo pia mabadiliko katika Utumishi wa Umma. 

Naibu Seif amefafanua mambo ya msingi iliyoisukuma Serikali kutayarisha na kutekeleza Mkakati wa Mabadiliko katika Utumishi wa Umma  kuwa ni pamoja na kuwepo kwa ishara zilizoleta   changamoto kubwa kipindi cha nyuma  ambazo zilipelekea kukwamisha utoaji wa huduma kisichoridhisha kwa wananchi katika kuleta ufanisi “suala hili lisipoangaliwa malengo ya maendeleo ya kuondosha umasikini hayataweza kufikiwa ”alisisitiza. 

Aidha amesema kutokuwepo kwa mgawanyo wa majukumu ulio muafaka baina ya Wizara na Idara, Taasisi zinazojitegemea za Serikali Kuu kwa upande mmoja , Malaka za Serikali za Mitaa kwa upande mwengine kumeviza uwezo wa vyombo hivi kuwahudumia wananchi ,vile vile uwezo mdogo wa watumishi wa umma, upungufu wa watumishi katika utumishi wa umma,viwango vya maslahi kwa watumishi kutokuwa muafaka , jambo lililofanya watu kutopenda kufanya  kazi katika utumishi wa umma.
 
Nae Mkurugenzi Mipango Sera na Utafiti wa Ofisi ya Rais Katiba Sheria Utumishi wa Umma na Utawala Bora Bi Daima Mohamed Mkalimoto  amesema madhumuni ya kikao hicho ni kutafakari kwa pamoja juu ya utekelezaji wa  mpango wa kuimarisha Utumishi wa Umma Zanzibar na kuelezea hali halisi ilivyo kwa sasa changamoto na hatimae kupokea maoni na michango itakayosaidia kuzingatiwa katika uandaaji wa program ya pili ya mabadiliko ya Utumishi wa Umma.
 
“Tukiwa ni watumishi wa Umma tunajukumu la kufanya kazi kwa kufuata Sera yetu inayotuongoza  hivyo kufanyakazi kwa uhakika kutaleta mageuzi” alisisitiza  na kusema kuwa Sera inatamka Dhima ya Utumishi wa Umma Zanzibar ni kutoa huduma bora kwa ufanisi na tija kwa umma wa Zanzibar na kwa kiwango cha juu cha uadilifu na heshima.



Baadhi ya mada zilizojadiliwa  ni pamoja na  usimamizi wa rasilimali watu,  usimamizi wa kumbukumbu na taarifa , serikali za mitaa  

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.