Habari za Punde

Mbunge na Mwakilishi wa Jimbo la Tunguu Zanzinar Wakabidhi Vifaa Vya Michezo Kwa Ajili ya Michezo ya Vijana Jimbo la Tunguu Zanzibar.

Mwakilishi wa Jimbo la Tunguu Zanzibar Mhe. Simai Mohammed Said, akizungumza na Vijana wa Jimbo la Tunguu Zanzibar, wakati wa hafla ya kukabidhi Seti 10 za Jezi kwa ajili ya Michguano ya Mchezo wa mpira Jimbo la Tunguu Zanzibar itakayowashirikisha Vijana wa Jimbo hilo. makabidhiano hayo yamefanyika katika Kituo cha Vijana Dunga Bweni Wilaya  ya Kati Unguja. 
Mwakilishi wa Jimbo la Tunguu Zanzibar Mhe. Simai Mohammed Said, akizungumza na Vijana wa Jimbo la Tunguu Zanzibar wakati wa hafla ya kukabidhi Seti za Jezi kwa ajili ya Michuano ya Kombe la Jimbo kwa Vijana wa Jimbo la Tunguu Zanzibar.Vifaa hivyo vya michezo vimetolewa na Mbunge na Mwakilishi  wa Jimbo la Tunguu Zanzibar.
Mwakilishi wa Jimbo la Tunguu Zanzibar Mhe. Simai Mohammed Said, akikabidhi Seti 10 za Jezi kwa Ajili ya Michuano ya Kombe la Jimbo litakalowashirikisha Vijana wa Jimbo la Tunguu Zanzibar.
Mwakilishi wa Jimbo la Tunguu Zanzibar Mhe. Simai Mohammed Said, akimkabidhi Seti ya Jezi Mwenyekiti wa Vijana Jimbo la Tunguu Zanzibar Ndg. Said Hassan na kulia Katibu wa Vijana Jimbo la Tunguu Ndg. Ali Khatib Mussa Kisu, makabidhiano hayo yamefanyika katika Kituo cha Vijana Dunga Bweni Wilaya ya Kati Unguja. 
Vijana wa Jimbo la Tunguu Zanzibar wakishangilia wakati wa hafla hiyo ya kukabidhiwa Vifaa vya Michezo kwa ajili ya Michuano yao ya Kombe la Jimbo la Tunguu Zanzibar.
Mwenyekiti wa Vijana wa CCM Jimbo la Tunguu Zanzibar Ndg. Said Hassan, akizungumza wakati wa hafla hiyo ya kukabidhiwa Vifaa vya Michezo kwa Ajili ya Michguano yao ya Jimbo la Tunguu katika mchezo wa mpira wa miguu.
Katibu wa Vijana wa CCM Jimbo la Tunguu Zanzibar Ndg. Ali Khatib Mussa akitowa shukrani kwa mchango wa Viongozi wa Jimbo lao ili kufanikisha Michuano yao ya Mpira wa Miguu ya Jimbo la Tunguu Zanzibar, hafla hiyo imefanyika katika Kituo cha Vijana na Maendeleo Dunga Bweni Wilaya ya Kati Unguja. 

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.