Habari za Punde

Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi Unguja Mhe. Ayoub Mohammed Mahmoud Akifungua Tamasha la Muziki wa Kizazi Kipya Zanzibar Viwanja Vya Magirisi leo.

Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi Ayoub Mohamed Mahmoud akimkabidhi zawadi ya Mbuzi Nahodha wa Timu ya Kijitoupele Khamis Hamadi  Khamis  kwa kuwa mshindi wa kwanza wa mpira wa miguu huko Uwanja wa Magirisi Wilaya ya Magharibi ‘B’ Unguja wakati wa Ufungaji wa Tamasha la Mapinduzi Safari la Miaka 55. 
Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi Ayoub Mohamed Mahmoud akitoa shukurani kwa Wasanii wa Zanzibar (Zanzibar Flever Unit) kwa kuandaa Tamasha la Mapinduzi Safari la Miaka 55  wakati akifunga Tamasha hilo katika Uwanja wa Magirisi Wilaya ya Magharib ‘B’ Unguja.  
Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi Ayoub Mohamed Mahmoud akikagua Timu za Mpira wa Miguu ya Wasanii na Kijitoupele katika Uwanja wa Magirisi Wilaya ya Magharibi ‘B’ Unguja katika Ufungaji wa Tamasha la Mapinduzi Safari la Miaka 55.
Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi Ayoub Mohamed Mahmoud akikagua Timu za Mpira wa Miguu ya Wasanii na Kijitoupele katika Uwanja wa Magirisi Wilaya ya Magharibi ‘B’ Unguja katika Ufungaji wa Tamasha la Mapinduzi Safari la Miaka 55. -Picha na Maryam Kidiko.

Na Mwashungi Tahir. Maelezo. 30-12-2018.
Msanii wa kizazi kipya Felista  Magindu (Lady Blach) amewaomba akinamama  wenye vipaji wajitokeze kwa wingi katika fani ya usanii wa Muziki ili viweze kuonekana.
Akizungumza na Waandishi wa habari huko Kiwanja cha Magirisi meli nne wakati wa ufungaji wa Bonanza la Wasanii wa kizazi kipya ikiwa ni miongoni mwa shamra shamra za Maadhimisho ya miaka 55 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar, ambapo kilele chake kitafanyika Kisiwani Pemba.
Amesema wapo akinamama wenye vipaji vya aina tofauti kama kuimba na kupiga Ala lakini wanashindwa kujitokeza kutokana na dhana potofu ya kuwa mziki ni uhuni.
“Naomba niwahakikishie kuwa Sanaa si uhuni ni ajira kama zilivyo ajira nyengine na kuwaombeni wanawake wenzangu mujitokeze kwa wingi katika matamasha na mambo mengine ili kuwaelimisha na kuwaburudisha wanajamii,” Alisema Ladya Block.
 Aidha aliwataka kuondosha imani potofu ya kuhisi kuwa wanawake hawana thamani katika jamii wanapoonekana kwenye Majukwaa wakiimba kwani ni mambo yaliyoanza zamani Zanzibar.
Lady Block aliwataja Wasanii maarufu wa zamani akiwemo Siti Binti Sadi na Fatma binti Baraka (Bi Kidude) kuwa waliipatia sifa kubwa Zanzibar, Tanzania na Afrika Mashariki kwa jumla.
“Kuna vipaji vya aina nyingi ya usanii Zanzibar ikiwemo kusuka, kuchora, michezo ya kuigiza, kuimba, ufinyanzi, kusuka mikoba na mikeka hali ambayo inawapatia ajira akina mama wengi hapa nchini,”Alisema Msanii huyo wa kizazi kipya.
Msanii mwengine wa kizazi kipya Sultani Abubakari (King) ameishukuru Serikali ya  Mapinduzi ya Zanzibar kwa kuwaunga mkono  na lengo la Tamasha la miaka 55 ya Mapinduzi ni kuhamasisha jamii umuhimu wa Mapinduzi hayo tokea yalipofanyika hadi tulipofikia.
Akifunga Tamasha hilo, Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi Ayoub Mohamed Mahmoud amewasa wasanii kujenga ushirikiano na kuwa kitu kimoja katika kuyalinda Mapinduzi ambayo yameleta amani na utulivu ndani ya visiwa vya unguja na pemba.
Mkuu wa mkoa alitumia nafasi hiyo kuwahimiza wananchi kujitokeza kwa wingi katika kampeni ya kuweka usafi tarehe 31, mwezi huu ambayo imeteuliwa kuwa siku ya rasmi ya uzinduzi wa shamra shamra za maadhimisho ya miaka 55 ya Mapinduzi ya Zanzibar.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.