Habari za Punde

Mwakilishi wa Jimbo la Tunguu Mhe. Simai Mohammed Said, Akitembelea Kikundi cha Vijana cha Maendeleo Dunga Wilaya ya Kati Unguja.

Mwakilishi wa Jimbo la Tunguu Zanzibar Wilaya ya Kati Unguja Mkoa wa Kusini Mhe. Simai Mohammed Said, akimksikiliza Katibu Uhamasishaji wa Kikundi cha Vijana cha Maendeleo Dunga Bweni Bi. Hawa Ali Mzee,akitowa maelezo ya moja ya bidhaa ya Shampoo inazozalishwa wakati wa kukitembelea kikundi hicho katika eneo lao la Kituo cha Elimu Dunga Bweni, kulia Mwenyekiti wa UVCCM Jimbo la Tunguu Ndg. Said Hassan na katikati Katibu wa UVCCM Jimbo la Tunguu Zanzibar Ndg. Ali Khatib Mussa (Kisu).
Mwakilishi wa Jimbo la Tunguu Zanzibar Mhe. Simai Mohammed Said akiwa na bidhaa aina ya Shampoo inayozalishwa na kikundi hicho wakati alipofanya ziara kutembelea na kujionea baadhi ya bidhaa mbalimbali zikiwemo Jiki, Shampoo, Mafuta ya mngando na Ushonaji wa Nguo na Mashaka.
Mwakilishi wa Jimbio la Tunguu Zanzibar Mhe. Simai Mohammed Said akizungumza na Viongozi wa Kikundi cha Vijana cha Maendeleo Dunga Bweni Wilaya ya Kati Unguja Mkoa wa Kusini Unguja.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.