Habari za Punde

Wananchi ,watumishi watakiwa kuripoti matendo yote yanayokwenda kinyume na maadili ya Taifa

Wananchi wa Mikoa Miwili ya Pemba pamoja na Watendaji wa Taasisi za Umma wakiandamana katika Maadhimishoya Siku ya Maadili na Haki za Binadamu zilizofanyika katika Uwanja wa Michezo Gombani Mpya.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akiyapokea Maandamano ya Wananchi wa Mikoa Miwili ya Pemba pamoja na Watendaji wa Taasisi za Umma katika Maadhimisho ya Siku ya Maadili na Haki za Binadamu.
Baadhi ya Viongozi, Watendaji wa Taasisi za Umma pamoja na Wananchi wakifuatilia matuykio mbali mbali yaliyojiri kwenye Maadhimishoya Siku ya Maadili na Haki za Binadamu.
Baadhi ya Viongozi, Watendaji wa Taasisi za Umma pamoja na Wananchi wakifuatilia matuykio mbali mbali yaliyojiri kwenye Maadhimishoya Siku ya Maadili na Haki za Binadamu.
Wasanii wa Kikundi cha Maigizo cha JUFE Film Production cha Mjini Wete wakitoa elimu ya mapambano dhidi ya Rushwa katika Igizo Maalum la kuadhimisha siku ya Maadili na Haki za Binadamau Gombani Mpya Chake chake Pemba.
Mwenyekiti wa Tume ya Maadili ya Viongozi wa Umma Nd. Assaa Rashid akisoma Risala kwenye Maadhimisho ya Siku ya Maadili na Haki za Binadamu.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Katiba Sheria na Utawala Bora Zanzibar Mh. Haroun Ali Suleiman akimkaribisha Mgeni Rasmi kuzungumza katika Kilele cha Maadhimisho ya Siku ya Maadili na Haki za Binadamu.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akiwahutubia Wananchi wa Pemba katika Kilele cha Maadhimisho ya Siku ya Maadili na Haki za Binadamu kilichofanyika katika Uwanja wa Michezo Gombani Mpya Mjini C hake Chake Pemba.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Katiba Sheria na Utawala Bora Zanzibar Mh. Haroun Ali Suleiman Kulia akimshindikiza Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi Kushoto baada ya kukamilika kwa sherehe za maadhimisho ya Siku ya Maadili na Haki za Binadamu.Picha na – OMPR – ZNZ.

Na Othman Khamis, OMPR
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi ametoa wito kwa Wananchi pamoja  na Watumishi wa Taasisi za Umma Nchini kuwa tayari katika kuyaripoti matendo yote maovu yanayoonekana kwenda kinyume na Maadili ya Taifa.
Alisema wapo baadhi ya Watu wachache wamekuwa wakirejesha nyuma jitihada zinazoendelea kuchukuliwa na Serikali katika mapambano dhidi ya Rushwa Watu wanaostahiki washughulikiwe kwa mujibu wa Sheria za Nchi bila ya huruma wala muhali.
Akizungumza na Wananchi katika Maadhimisho ya Siku ya Maadili na Haki za Binaadamu katika Kiwanja cha Michezo Gombani Chake Chake Pemba Balozi Seif Ali Iddi alisema tatizo la Rushwa katika Jamii na mgongano wa Kimaslahi yanaendelea kuathiri Nchi nyingi Duniani ikiwemo pia Tanzania.
Balozi Seif alisema  vitendo hivyo hudhoofisha upatikanaji wa Haki za Binaadamu kwa kiwango kikubwa na kurejesha nyuma jitihada za kuimarisha misingi ya Haki na Utawala Bora.
Alisema ni jambo la faraja kwamba kupitia zijitahada zinazochukuliwa na Serikali zote mbili Nchini, ile na Jamuhuri na ya Mapinduzi ya Zanzibar Tanzania ni miongoni mwa Nchi zinazofanya vizuri katika masuala ya Utawala Bora na kupinga Rushwa.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar alisema ripoti iliyotolewa Mwaka  2017 inayoangazia mapambano dhidi ya Rushwa inaonyesha Tanzania kuwa ni Nchi ya Pili ndani ya Ukanda wa Afrika Mashariki ikitanguliwa na jirani yake Rwanda katika mapambano dhidi ya Rushwa.
Balozi Seif alisema kwa upande wa Kimataifa Tanzania inashikilia nafasi  ya 103 kutoka nafasi ya 116 ambapo aliwashauri Wananchi kuunganisha nguvu za pamoja na Serikali katika mapambano dhidi ya Rushwa ili kujiwekea nafasi ya kufanya vizuri katika ripoti itakayotolewa Mwaka 2018.
Alifahamisha kwamba Tanzania iliamua kuweka ulinzi wa Haki za Binaadamu katika Katiba yake na kupelekea kupiga hatua kubwa katika kuyatekeleza malengo ya Umoja wa Mataifa kufuatia kuridhia Mikataba mbali mbali ya Taasisi hiyo ya Kimataifa.
Aidha alisema Katiba ya Zanzibar ya Mwaka 1984 imelipa umuhimu mkubwa suala la mapambano dhidi ya Rushwa katika kifungu chake cha  10{b} kinachokataza na kukemea kabisa vitendo vya Rushwa na utumiaji mbaya wa cheo au madaraka dhidi ya Umma.
Makamu wa Pili nwa Rais wa Zanzibar aliwanasihi wasimamizi wa Tenda ye yote ile kuwa makini katika kusimamia haki na Uadilifu kwa wanaoomba sambamba na kuepuka kuitia hasara Serikali Kuu kutokana na tabia ya baadhi ya Watu kuongeza chao.
Akizungumzia vitendo vyengine viovu vya utoaji wa Mimba ambavyo baadhi ya wakati hushamiri ndani ya Jamii Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif  alisema kimsingi vitendo hivyo vinavunja Haki ya kuishi ya  kiumbe kilicho kuwemo ndani ya Tumbo la Mama ambacho hakina hatia yoyote ile.
Balozi Seif alieleza kwamba vitendo hivyo kwa bahati mbaya si mara nyingi kuzungumzwa katika majukwaa lakini vipo na pengine vinaongezeka kwa kasi vikiwahusisha zaidi Madaktari waliokosa maadili ya kazi.
Alisema wakati Jamii inaadhimisha siku hii ya maadili na Haki za Binaadamu ni vyema kwa Wananchi wakadhamiria kikweli kupiga vita kasoro hii Nchini ambayo mbali ya kumpoteza maisha ya kiumbe kilicho tumboni lakini hata maisha yua mja mzito mwenyewe yanakuwa hatarini.
Akisoma Risala Mwenyekiti wa Tume ya Maadili ya Viongozi wa Umma Nd. Assaa Rashid alisema misingi ya Utawala Bora itaimarika zaidi iwapo Jamii itajikita katika kuziba Mianya ya Rushwa na kuongezeka kwa Uwajibikaji.
Nd. Assaa alisema Maadhimisho ya Siku ya Maadili na Haki za Binadamu  ni muhimu kwa vile husaidia Jamii kuelewa dhana ya Utawala Bora ambayo ni sahihi katika mazingira yao ya kujipatia Haki zao.
Alisema yapo mafanikio makubwa yaliyopatikana tokea kuasisiwa kwa Tume ya Maadili ya Viongozi wa Umma kutokana na mipango imara inayowaongoza Watendaji wa Taasisi hiyo kutoa Elimu kwa Umma iliyochangia kuongezeka kwa uelewa wa Wananchi.
Mwenyekiti huyo wa Tume ya Maadili ya Viongozi wa Umma alivipongeza Vyombo vya Habari Nchini kwa mchango wake wa kushirikiana na Taasisi hiyo katika kuwapatia Taaluma Wananchi kupitia Redio, Magazeti, Matangazo na hata Vipeperushi tofauti.
Akimkaribisha Mgeni rasmi kwenye kilele cha Maadhimisho hayo ya Siku ya Maadili na Haki za Bianaadamu Waziri wa Nchi Ofisi yua Rais, Katiba, Sheria na Utawala Bora Mh. Haroun Ali Suleiman aliwaomba Watendaji wanaosiamamia Suala la Maadili kuwa na Lugha nzuri katika kuuhudumia Umma.
Waziri Haroun alisema  Wzaiara hiyo itaendelea kusimamia majukumu yake bila ya upendeleo Mtu au upande wowote, na kamwe haitakuwa tayari kumtetea Mtu atakayekiuka Maadili kwa kisingizio cha kujuana.
Mapema Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif aliyapokea Maandamano ya Taasisi mbali mbali zinazosimamia Maadili na Haki za Jamii pamoja na Wananchi katika kuadhimisha sherehe hizo.
Ujumbe wa Mwaka huu wa Siku ya Maadili na Hali za Binadamu unasema “ Tuimarishe Uadilifu, Uwajibikaji, Haki za Binadamu na Mapambano dhidi ya Rushwa kwa Maendeleo ya Taifa.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.