Habari za Punde

Kongamano la 6 la Vijana Kuzungumza Vijana na Mapinduzi. Kuadhimisha Miaka 55 ya Mapinduzi ya Zanzibar.

NAIBU katibu Mkuu Wizara ya Vijana Utamaduni Sanaa na MIchezo Zanzibar, Amour Hamil Bakari akiwangoza viongozi wa mabaraza ya Vijana katika kuimba wimbo wa taifa wa Zanzibar, wakati wa kongamano la 6 kuelekea maadhimisho ya miaka 55 ya Mapinduzi, huko katika ukumbi wa baraza la mji chake chake
BAADHI ya Vijana kutoka mabaraza ya Vijana ya mikoa miwili ya Pemba, wakiimba wimbo wa Zanzibar wakati wa kongamano la 6 kuelekea maadhimosho ya Miaka 55 ya Mpinduzi Matukufu ya Zanzibar, huko katika ukumbi wa baraza la mji Chake Chake.
NAIBU katibu Mkuu Wizara ya Vijana Utamaduni Sanaa na Michezo Zanzibar Amour Hamil Bakari, akizungumza katika kongamano la sita kuelekea maadhimisho ya sherehe za Mapinduzi Matukufu ya zanzibar kwa mabaraza ya Vijana, huko katika ukumbi wa baraza la Mji Chake Chake.
MKUU wa Wilaya ya Kaskazini B Unguja Rajab Ali Rajab, akifungua kongamano la 6 kuelekea maadhimosho ya Miaka 55 ya Mpinduzi Matukufu ya Zanzibar, huko katika ukumbi wa baraza la mji Chake Chake.
Muwailishaji wa Mada ya Kwanza Msham Abdalla Khamis, juu ya Historia ya Zanzibar kabla ya Mapinduzi Matukufu ya mwaka 1964, kwa wajumbe wa mabaraza ya Vijana huko chake chake kuelekea maadhimisho ya Mapinduzi ya Zanzibar. 

VIONGOZI wa Mabaraza ya Vijana kutoka Kisiwani Pemba, wakifuatilia kwa makini ufunguzi wa kongamano la 6 kuelekea maadhimosho ya Miaka 55 ya Mpinduzi Matukufu ya Zanzibar, huko katika ukumbi wa baraza la mji Chake Chake.
(Picha na Abdi  Suleiman - Pemba)

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.