Habari za Punde

Mhandisi wa Wilaya na Mkandarasi Waliomdanganya Naibu Waziri wa Maji,Mhe.Juma Aweso,Watupwa Mahabisu.

Naibu Waziri wa Maji na Umwagiliji,Juma Aweso akitizama namna mafundi wakiunganisha Bomba za Maji  katika mradi unaopeleka maji katika Kata ya Sopeko kikiwemo kijiji cha Lendikinya wilayani Monduli katika mkoa wa Arusha.
Mafundi wakiendelea na uunganishaji wa Bomba za kupeleka Maji katika kijiji cha Lendikinya wilayani Monduli mkoa wa Arusha.
Mhadisi wa Maji wa wilaya ya Monduli Charles Seidea akimueleza Naibu Waziri wa Maji ,Juma Aweso kuhusu namna mradi huo ulivyotekelezwa katika kijiji cha Lendenyika wilayani Monduli.
Baadhi ya Wananchi katika kijiji cha Lendenyika wilayani Monduli wakimsikiliza Naibu Waziri wa Maji na Umwagiliaji Juma Aweso (hayupo pichani) alipotembelea mradi huo kujionea maendeleo yake.
Naibu Waziri wa Maji na Umwagiliaji ,Juma Aweso akiwa ameongozana na Mbunge wa jimbo la Monduli ,Julius Kalanga pamoja na wananchi wakienda kujionea namna mkandarasi alivyopitisha Bomba za Plastiki kwenye Korongo badala ya Bomba za Chuma.
Naibu Waziri wa Maji na Umwagiliaji ,Juma Aweso akitizama Bomba za Plastiki zilizopitishwa katika Makorongo badala ya Bomba za Chuma katika mradi wa maji wa kusaidia vijiji 10 vya kata ya Sopeko wilayani Monduli.
Baadhi ya Bomba za Plastiki zikiwa zimepita kwenye Korongo badala ya Bmba za Chuma .
Askari Polisi akiwa amewashikilia ,Mhandisi wa Maji wa wilaya ya Monduli,Charles Saidea (kulia) na Mkandarasi ,Ayo Jeremia wa kampuni ya Meru Constructions mara baada ya Naibu Waziri kuamuru wakamatwe kutokana na kubainika kufanya udanganyifu katika mradi huo.
Mhadisi wa Maji wa wilaya ya Monduli,Charles Saidea akiingia kwenye gari la Polisi mara baada ya kushikiliwa kwa amri ya Naibu Waziri wa Maji na Umwagiliaji ,Juma Aweso baada ya kubaini kuwepo kwa udanganyifu katika mradi wa Maji unaendelea katika kijiji cha Lendenyika wilayani Monduli.
Mkandarasi ,Ayo Jeremia wa kampuni ya Meru Constructions akiingia kwenye gari la Polisi mara baada ya kushikiliwa kwa amri ya Naibu Waziri wa Maji na Umwagiliaji ,Juma Aweso baada ya kubaini kuwepo kwa udanganyifu katika mradi wa Maji unaendelea katika kijiji cha Lendenyika wilayani Monduli.
Mkandarasi ,Ayo Jeremia wa kampuni ya Meru Constructions pamoja na Mhandis wa Maji wa wilaya ya Monduli ,Charles Saidea wakiwa kwenye gari la Polisi mara baada ya kushikiliwa kwa amri ya Naibu Waziri wa Maji na Umwagiliaji ,Juma Aweso baada ya kubaini kuwepo kwa udanganyifu katika mradi wa Maji unaendelea katika kijiji cha Lendenyika wilayani Monduli.
Baadhi ya wananchi katika kijiji cha Lendenyika wakishuhudia wakati watalaamu hao wakichukuliwa katika gari la Polisi.


Na.Dixon Busagaga,Monduli.
NAIBU Waziri wa Maji na Umwagiliaji ,Juma Aweso ameamuru kukamatwa na kuwekwa mahabusu kwa Mhandisi wa Maji wa wilaya ya Monduli ,Charles Saidea na Mkandarasi kutoka kampuni ya Meru Constructions ,Ayo Jeremia kwa tuhuma za kufanya udanganyifu katika miradi wa maji inayoendelea katika vijiji 10 vya Halmashauri ya wilaya ya Monduli .

Waziri Aweso ametoa agizo hilo katika kijiji cha Lendinyika wakati wa ziara yake ya siku moja katika wilaya ya Monduli kukagua utekelezaji wa Miradi ya Maji katika vijiji 10 vya Halmashauri hiyo,ziara  ambayo hata hivyo alilazimika kuikatisha mara baada ya kubaini  kuwepo kwa taarifa zinazo kinzana na taarifa ya utekelezaji wa mradi wa maji wenye thamani ya Sh Bil 1 na Mil 79 .

Mbali na uwepo wa dosari nyingi za kiufundi ,mradi huo unaotajwa kukamilika kwa asilimia 85 bado haujaanza kutoa maji huku Mkandarasi akieleza kuidai Serikali sehemu ya fedha za mradi hu jambo ambalo Mhandisi alionekana kupinga uwepo wa madai hayo.

Hoja ya kuwepo kwa Mabomba ya plastiki yaliyopita katika Makorongo iliibuliwa na mmoja wa wakazi wa kijiji cha Lendikinya Lemta Naisikie baada ya kutaka kujua kama ni sahihi kwa mkandarasi kupitisha Bomba hizo katika sehemu za wazi badala ya bomba za chuma.

“Swali langu ni moja ,Bomba zilizotandazwa kuleta maji katika kisima kuu  ,kuna sehem za Makorongo zote zimewekwa hii bomba la mpira ,hii naona ni changamoto afadhali ingewekwa bomba la chuma na maeneo mengine kuna mawe tungeomba mkandarasi atandaze bomba la chuma ili zisilete athari baadae”alisema Naisikie.

Baada ya kutolewa kwa hoja hiyo Naibu Waziri ,Aweso aliamua kutembelea baadhi ya Makorongo na kujionea Bomba la Plastiki likiwa limepita juu badala ya Bomba la Chuma ndipo akaamua kutoa maelekezo .

“Viongozi wenu wote wanazungumzia swala la maji ,Lendikinya ni moja ya vijiji vyenye changamoto kubwa sana ya maji ,Mbunge wenu amepiga sana kelele kuhusu maji kwa wananchi wa Monduli,sasa sisi leo tumekuja hapa tumeona kuna mradi wa zaidi ya sh Bil 1 na Mil 79 lakini mradi uko zaidi ya asilimia 80 lakini maji kwa wananchi hakuna .”alisema Aweso 

“Unawauliza wataalamu wetu wakupe taarifa zile sahihi ,hawakupi ,leo mwananchi huyu wa kawaida kabisa anakupa taarifa sahihi mahala ambapo yalitakiwa kuwekwa mabomba ya chuma yameweka mabomba ya plastiki na hakuna usimamizi wa iana yoyote .”aliongeza Aweso.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.